Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
SHULE ya Sekondari Magoza iliyopo Kata ya Kisukuru wilayani Ilala, wajivunia mafanikio kitaaluma inafanya vizuri katika matokeo mbali mbali ya mitihani ya kuhitimu kidato cha nne.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo, Bonna Mushi, katika mahafali ya 14 ya kidato cha nne ambapo wanafunzi 250 wasichana 97 wavulana 153 walihitimu na kukabidhiwa vyeti na Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala RUKIA MWENGE .
“Tunajivunia mafanikio kitaaluma katika shule yetu ya Magoza Sekondari mwaka 2022 wanafunzi 380 walifanya mitihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kati yao wanafunzi 49 waliochaguliwa kidato cha tano ,wanafunzi 24 walikwenda vyuo mbali mbali vya Serikali na wanafunzi 177 wana sifa za kujiunga vyuo “alisema Mushi.
Mkuu Bona Mushi ,alisema shule hiyo imeweza kushiriki katika mashindano mbali mbali kitaaluma nje ya shule na kupata tuzo mfano mwaka 2019 walishiriki mashindano ya somo la Hisabati na kuibuka washindi na kuzawadiwa vitabu 70 vya somo hilo na mwaka huu 2023 wanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha tatu walifanya vizuri katika mitihani yao ya wilaya na kupewa zawadi mbali mbali.
Akizungumzia sekta Michezo alisema pia wanang’ara katika michezo ya umoja wa shule za Sekondari UMISSETA na mashindano ya Afrika Mashariki na kati (FEASA )ambapo katika UMISSETA wanafunzi wa kidato cha tatu wa Magoza walifanya vizuri katika riadha na kuibuka kidedea kushika nafasi ya tatu UMISSETA Taifa Mwajuma Mussa Mkuta, ambapo mpaka sasa amefikisha medali saba zingine za mashindano ya kimataifa.
Wakati huo huo alisema anaishukuru Serikali ya chama cha Mapinduzi CCM inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wa Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule ya sekta ya Elimu na kujenga shule nyingi sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Aidha alisema pia Diwani wa kata ya Kisukuru Lucy Lugome amewajengea ukuta kwa kushirikiana na wananchi wapenda maendeleo ambapo alisema ujenzi wa ukuta huo umesaidia kuimarisha usalama wa shule hiyo na umedhibiti utoro kwa wanafunzi.
Katika hatua nyingine alisema shule hiyo imefadhiliwa kwa kufanyiwa utarabati vyumba vitatu vya madarasa,ambapo kwa sasa vinatumika kwa ajili ya maktaba, ofisi ya walimu na chumba cha kupikia (Cooker room)kwa ajili ya masomo ya upishi food and nutrition wanashukuru Kampuni ya AECI Mining Company kwa ufadhili huo ambapo kutokana na kujitoa kampuni hiyo imekabidhiwa cheti cha shukrani kwa kutambua mchango wao katika kuisaidia Serikali cheti hicho kimekabidhiwa na Diwani Lukia Mwenge kwa niaba ya Diwani wa Kisukuru Lucy Lugome.
Muhitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo Salama Ngoma,alisema changamoto kubwa ya shule hiyo ukosefu wa maji safi ya DAWASA ambapo alisema changamoto hiyo kubwa inawasili kitaaluma kwani baadhi ya masomo ya vitendo huitaji maji safi ya DAWASA pia ulazimika kununua maji ya kunywa wakati wote wawapo shuleni.
Mwanafunzi Salama Ngoma, alisema ombi lao kwa wadau wa elimu wawapatie mashine kubwa ya Photocopy mashine kwa ajili ya kurudufu mitihani yao ya kujipima ya majaribio kila mwezi.
Meneja Mwajiri wa AECI Mining Company Jaques Botha ,alipongeza Serikali na uongozi wa shule hiyo kuwapa cheti cha kutambua mchango wao,ambapo pia wakitoa ahadi ya kukarabati ofisi ya mkuu wa shule na kuwa ya kisasa .
Aliwataka wahitimu hao wa kidato cha nne kujiandaa na mitihani yao vizuri huku wakimtanguliza mwenyezi Mungu ili waweze kufanya vizuri mitihani yao wajiandae na vyuo .
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua