January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya sekondari Juhudi wajivunia sekta Michezo

Na Heri shaban, TimesMajira Online

SHULE ya sekondari ya Juhudi iliyopo Wilayani Ilala jimbo la Ukonga inajivunia katika sekta ya Michezo imeweza kuitangaza wilaya ya Ilala pamoja na Tanzania katika mashindano ya shule za Afrika Mashariki ambapo katika michezo ya Basketball Mwezi Agosti mwaka huu walikwenda kushiriki mashindano hayo na kufanya vizuri.

Akizungumza wakati wa Mahafari ya kumi na tisa ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo Mkuu wa shule hiyo Happiness Pallangyo, alisema shule ya sekondari Juhudi ina wanafunzi wenye vipaji kwani wanajivunia shule hiyo inafanya vizuri katika sekta ya Michezo.

“Mwezi Agosti mwaka huu 2023 shule imewakilisha Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki katika michezo ya Basketiball shule yetu imeelekeza bidii kubwa katika michezo mbalimbali kama mpira Pete,mpira wa meza ,riadha na mpira miguu ,mpira kikapu,basketball “alisema Pallangyo.

Mwalimu Pallangyo, alisena michezo mingine ambayo wamejikita nayo na shule hiyo inafanya vizuri Amerikan Foot ball,kabadi,Rubby ambapo alisema wanafunzi wanashiriki katika ngazi mbalimbali za kimashindano .

Aidha alisema katika mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari (UMISSETA ) Taifa wanafikia kunyakuwa medali katika michezo mbalimbali kutokana na wachezaji wengi wanavipaji ambapo UMISSETA Taifa mwaka 2023 wanafunzi watatu walishiriki walitoka Juhudi Sekondari.

Mwalimu Pallangyo alisema pia mwanafunzi Mmoja wa Juhudi sekondari aliteuliwa kwenda kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki jijini Nairobi Kenya na muhitimu wa mwaka 2017 Jesca Ngisaise, alichaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18.

“Shule yetu ya Juhudi sekondari aipo nyuma pia katika mpira wa kikapu nchini Afrika Kusini tulifanikiwa kupata ufadhili wa kucheza mpira wa kikapu na taaluma ya mpira wa kikapu nchini Senegal “alisema