November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya msingi uhuru wasichana wajivunia mafanikio

Na Herishaban, TimesMajira Online

Shule ya Msingi Uhuru wasichana wajivunia mafanikio kitaaluma inafanya vizuri katika mitihani mbali mbali ya ndani na nje na kuwawezesha kupata ufaulu wa asilimia 100 kila mwaka.

Akizungumza wakati wa Mahafari ya Darasa la saba leo mwalimu mkuu wa shule hiyo Neema Mtachi,alisema shule hiyo ya uhuru wasichana imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya Mock wilaya na Mock Mkoa na matumaini yao watapa matokeo mazuri ya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi .

“Tunajivunia kitaaluma katika shule yetu ufaulu kila mwaka tunafaulisha kwa asilimia 100 ikiwemo mwaka 2021 mpaka 2022 wanafunzi wote wamefaulu wameenda kidato cha kwanza kwani shule yetu ina mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na walimu na wanafunzi wanajitahidi kuyaweka katika hali nzuri na kupata ushindi sekta ya mazingira “alisema Neema .

Wakati huo huo Mwalimu Neema alimpongeza Mbunge wa Jimbo Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu , kutoa shilingi millioni kumi kwa ajili ya kutengeza vyoo vya Shule ya uhuru wasichana.

Alisema Mbunge Zungu ametatua changamoto ya vyoo vya shule hiyo ya Uhuru wasichana vitakarabatiwa na kuwa vyoo vya kisasa .

Aidha alimshukuru Mlezi wa shule hiyo mfanyabiashara Thomas Limo ameunga mkono juhudi za Serikali amechangia madawati 50 katika shule hiyo kwa ajili ya wanafunzi kukalia.

Akizungumzia wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu shuleni hapo aliwataka wawe na nidhamu huko wanapoenda waende kuipeperusha vizuri bendera shule ya msingi uhuru wasichana shule pekee ya Wanawake Tanzania.

Akizungumzia mmomonyoko wa maadili aliwataka Wazazi kuchunga watoto wao pia wasiruhusu wageni kulala chumba kimoja na watoto wajali usalama kwanza wa watoto wao Dunia imebadirika .

Kaimu Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Teddy Ngeiyamu aliwataka wahitimu hao wa Darasa la saba Uhuru wasichana wawe kioo cha jamii huko wanapoenda wakasome kwa bidii ili wawe viongozi wa Taifa la kesho .

Alipowapongeza walimu wa shule hiyo kukuza taaluma shuleni na kufanya vizuri katika masomo yao na mitihani mbali mbali.