Na Heri Shaaban, TimesMajira Online,Ilala
Shule ya Msingi Kisutu iliyopo wilayani Ilala Serikali imeipandisha hadhi mwaka huu kutoka kufundisha lugha ya Kiswahili sasa hivi wanafunzi wote wanafundishwa kingereza .
Akizungumza wakati wa Mahafari ya Darasa la saba shule ya Msingi Kisutu ambapo jumla ya wanafunzi 186 walimaliza darasa la saba mwaka huu 2023, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Elizabeth Masawe, alisema shule hiyo wamepata mafanikio makubwa katika kubadili lugha ya kujifunzia na ufundishaji kutoka Kiswahili kuwa ya Kingereza kwa mwaka wa masomo 2023 kuendelea yaani English Medium
“Tunajivunia mafanikio ya shule yetu tumepata mafanikio makubwa kitaaluma inafanya vizuri kila mwaka wanafunzi wanafaulu asilimia 100 wote wanaenda sekondari niushirikiano mzuri wa Walimu ,Wazazi na wanafunzi katika yetu “alisema Masawe.
Mwalimu Masawe alisema mwaka 2020 wanafunzi 188 walifanya mitihani wa kuhitimu elimu ya msingi wote asilimia 100 wamefaulu, mwaka 2021 wanafunzi 200 walifanya mitihani wa kuhitimu elimu ya msingi wote wamefaulu na mwaka 2022 idadi yao walikuwa wanafunzi 262 pia walifaulu wote yote ni kutokana na mazingira mazuri ya kufundishia yaliopo katika shule hiyo .
Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika sekta ya Elimu
Mwenyekiti wa chama cha Mapunduzi CCM Kata ya Kisutu Murtaza Darugar, aliwaasa wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo alisema elimu aina mwisho wala aina umri ,hivyo aliwataka wakienda nyumbani wasibweteke wakaenda katika makundi yasiofaa badala yake wakajisomee wasubiri matokeo yao .
Mwenyekiti Murtaza aliwataka Wazazi kuwa karibu na watoto Dunia sasa hivi imebadirika wasiingie katika mmomonyoko wa maadili badala yake wajiandae kwa ajili kujiandaa na kidato cha kwanza mwaka 2024 .
Aliwataka wanafunzi wa shule hiyo waliomaliza darasa la saba huko wanapoenda wawe kioo cha jamii wakaitangaze Kisutu , waige mfano Diwani wa kata ya Kisutu pamoja na Mwenyekiti wa Mtendeni wote wamesoma shule ya Kisutu .
Wakati huo huo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri wamewekeza sekta ya Elimu pamoja na sekta ya afya .
Pia alisema Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu amefanya mambo makubwa katika jimbo hilo kuboresha miundombinu ya elimu na Barabara .
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best