Na Mwandishi wetu ,timesmajira, Dar es SalaamÂ
SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA),limesema kuwa kila taasisi yenye waajili kuanzia 20 kati yao asilimia tatu wanapaswa kuwa watu wenye ulemavu kama sheria inavyobainisha.
Akizungumza katika mafunzo kwa njia ya mtandao jana yaliyotolewa na Wakili wa Shirikisho hivyo kwa waandishi wa habari,Novatus Rukwago alisema katiba inaeleza bayana mwajili kuhakikisha anaweka mazingira rafiki kwa mtu mwenye ulemavu.
Amesema waajili wote nchini wanapaswa kila mwaka kutoa taarifa kwa kamishna wa kazi juu ya hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika taasisi yake na hawa watu wenye ulemavu waliopata ajira kuwekewa  ulinzi wa kulindwa na kuhakikisha wanakuwa na mazingira mazuri ya kuendelea na kazi zao.
“Mafunzo haya yanalenga ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika ajira,hivyo mafunzo haya yanawakumbusha waandishi wa habari katika kufanya kazi zao kama wasemaji wa wasio na sauti kusaidia kutoa taarifa kwa wafanya maamuzi,”amesema na kuongeza
“Pia kuhakikisha uelimishaji wa haki na mahitaji kwa watu wenye ulemavu kwani wao wanaimani kwa waandishi wa habari kuwa ni waelimishaji wa haki na mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kuwasaidia kwenye mambo mbalimbali,”amesema
Amesema bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu katika ajira ikiwemo mifumo ya ajira bado haijawa jumuishi kwao hususani katika upande wa utangazaji wa ajira,usaili na sehemu zenyewe za ajira.
“Bado waajiliwa hawana uelewa wa kutosha kutokana na kuwa na hofu inayotokana na hisia badakla ya uhalisia huku utekelezaji wa sheria hauna usimamizi madhubuti ya utekelezaji wa kipengele cha ajira,”amesema na kusisitiza
“Pia kukosekana kwa Mkakati wa Wizara inayohusika na ajira ya namna gani wanaweza kuifikia asilimia tatu ya kuajili watu wenye ulemavu,”amesema Rukwago
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi