Na Irene Clemence, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), Mkoa wa Dar es Salaam, Namoto Yusuph Namoto amewasihi wamachinga wanaofanya shughuli zao katika Mkoa huo, kutokuwa sehemu ya uchomaji moto masoko kwasababu kufanya hivyo kunaisababishia Serikali hasara.
Namoto ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema baadhi ya wamachinga wasio waaminifu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uchomaji moto masoko.
“Nawaomba wamachinga wezangu tusiwe sehemu ya uchomaji moto masoko katika baadhi ya maeneo unakuta ni sisi au mtu mmoja mmoja au mwingine unakuta mtu amechukua mkopo sehemu ameshidwa kulipa anaona bora achome moto soko lionekane soko liliugua lengo aweze kupata madai ya bima,”amesema Namoto.
Ameendelea kueleza kuwa masoko hayo yamekuwa yakijengwa na Serikali lakini mnufaika mkubwa amekuwa ni mfanyabiashara ambaye amekuwa akiyatumia kupitia bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiuza.
“Nawaomba masoko haya tuyalinde na tutegeneze kamati zetu na vikosi vya ulinzi na kuhakikisha anakuwa ulinzi imara ili yoyote miongoni mwetu atakayebainika kuwa na nia ovu aweze kudhibitiwa Kwa mustakabali mpana wa Taifa letu,”alisisitiza Namoto.
Aidha amesema katika kidhibiti vitendo hivyo kwa sasa wamekuwa wakitekeleza kampeni maalumu inayojilikana kwa jina la udhibiti moto katika masoko lengo kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto katika masoko.
Amesema kupitia kampeni hiyo wameweza kuingia makubaliano na Benki ya maendeleo kwa ajili ya kuwapatia wamachinga bima za afya, bima ya maisha pamoja na bima za biashara kwa njia ya mkopo .
Mwenyekiti huyo amesema jambo la utoaji bima kwa wajasiliamali limekuwa ni kipaumbele katika chama hicho kwasababu lengo nikumuinua mjasiliamari mdogomdogo.
Akitaja masoko ambayo yamekuwa yakinufaika na elimu hiyo ni soko la mchikichini, soko la tazara, soko machinga comprex,soko la feri, soko la vetenari, soko la Tungi Kigamboni, soko la Kizuiani, soko la Tegeta Nyuki, pamoja na soko Magomeni.
“Wajibu wetu ni kuhakikisha mfanyabiashara anakuwa na bima zote pia tumeandaa mpango wa kuwafikia wajasiliamali ambao utausisha
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ili kuwarahisishia kupata huduma “amesema Namoto
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano