Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) limesema,kwa kushirikiana na serikali wapo katika mchakato wa kuhakikisha vyuo vya maendeleo ya Wananchi hapa nchini ,vinapata walimu wa masomo ya sekondari ili wanafunzi wanaorudia baada ya kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Hayo yamesemwa na Afisa Mawasiliano wa KTO Symphrose Makungu wakati akizungumza na waandishi walipotembelea katika banda lao kwenye maonyesho ya wiki ya Ubunifu yanayoendelea jijini Dodoma.
Alisema,Shirika hilo linalofanya kazi na vyuo vya Maendeleo ya Jamii hapa nchini limetoa fursa ya wanafunzi waliokatisha masomo kupitia programu ya Elimu Haina Mwisho kupata elimu ya sekondari bure kupitia mfumo usio rasmi wa elimu lakini changamoto ya ukosefu wa walimu wa masomo ya sekondari imekuwa ikichangia wanafunzi hao kushindwa kufanya vizuri pindi wanapohitimu kidato cha nne.
“Tunazo programu tatu ikiwemo ya Elimu haina mwisho ambayo ni kwa ajili ya , kuendeleza maarifa kwa wanawake na wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito,utoro,kushindwa kulipa ada ili waweze kutimiza malengo ya kielimu na kufikia ndoto zao za kimaisha .”alisema Makungu
Aidha alisema,wawapo chuoni watasoma na masomo mengine kama ujasirimali,masomo ya ufundi na stadi za maisha na kwamba lengo kubwa la programu ni kuhakikisha binti anafikia malengo yake ikiwa ni kujiajiri au kukabili ushindani katika soko la ajira na mwisho wa siku kumudu kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Kwa mujibu wa Makungu,changamoto nyingine ni wengi wanaorudi baada ya kukatisha hawafanyi vizuri katika mtihani wa mwisho kutokana na kutojitambua kwa maana wengi kurudi na tabia zile zile za awali zilizosababisha wakatishe masomo yao huku akisema wengine wanapata mimba nyingine huko huko vyuoni.
“Hata hivyo ili kukabiliana na changamoto hii tunaendelea kuwapa elimu ili waweze kujitambua na kuitumia fursa hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia
Hata hivyo alisema,tangu programu hiyo imeanza mpaka sasa zaidi ya mabinti 9,000 wamenufaika nayo huku akisema kwa mwaka huu peke yake walioingia kwenye programu hiyo ni wasichana wapatao 1,267 .
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini