January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shinini Mwenyekiti UWT, Simanjiro

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania UWT Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamemchagua Anna Shinini kuwa Mwenyekiti wa UWT wa Wilaya hiyo Kwa kupata kura 137.

Akitangaza Matokeo hayo mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Wilaya ya Simanjiro, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo amemtangaza Anna Shinini kuwa ndiye mshindi wa nafasi hiyo kwa kura 137 kati ya kura 221.

Aidha Makota amesema idadi ya wapiga kura umla walikuwa 223 ila kura 2 zimeharibika huku kura halali zilikuwa 221, ambapo wagombea walikuwa wawili Agnes Brown amepata kura 84 na huku Anna Shinini akiwa amepata kura 137.

” Kwa mamlaka niliyopewa juu ya Uchaguzi huu wa UWT ninamtangaza kwenu kuwa Anna Shinini ndiye Mwenyekiti wa UWT wa wilaya ya Simanjiro,” amesema Makota

Akizungumza baada ya kushinda nafasi hiyo Shinini amewashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kushika nafasi hiyo, huku akisema ameishiwa maneno makubwa ya kuzungumza dhidi ya kuwashukuru Kwa kumuamini.

Shinini amesema idadi ya kura alizopata inadhihilika kuwa hitaji lao lilikua ni yeye kuwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, hivyo ameiomba apewe ushirikiano mkubwa na hatimaye waweze kufanya kazi Kwa maslahi mapana ya UWT Wilaya ya Simanjiro.

Amesema yote aliyoyaahidi atahakikisha anayasimamia kikamilifu ili kuweza kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele na si vinginevyo.

” Ndugu zangu kupata hizi kura sio ufahari, kikubwa ni kumshukuru Mungu Kwa kunipa hii nafasi, hivyo basi Kwa kuwa uchaguzi umeshapita hivyo hivi sasa tujipange kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu ipasavyo kama tulivyoahidi” amesema Shinini.

Hata hivyo, Agnes amekubali matokeo hayo na kudai kuwa asiyekubali kushindwa siyo mshindani, ambapo amesema atahakikisha anatoa ushirikiano wake wa dhati iwapo utahitajika.Awali, uchaguzi wa UWT wilaya ya Simanjiro ulifanyika Septemba 24 mwaka huu ambapo kwa nafasi hiyo ya Mwenyekiti ililazimika kurudiwa mara mbili, nankuonekana kistahili kurudiwa upya.

Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Simanjiro Leocadia Fisoo amewashukuru Wajumbe wote wa UWT Wilaya ya Simanjiro kwa kuhudhuria kikamilifu Uchaguzi huo uliorudiwa.Fisoo alimpongeza Mwenyekiti huyo mpya wa UWT Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Anna Shinini Kwa ushindi alioupata na kumtakia kila la heri katika kutekelezwa hayo majukumu yake mapya.

Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa UWT Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Anna Shinini aliyepata kura 137 kati ya kura 221, kulia ni Agnes Brown aliyepata kura 84, kwenye Uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro uliofanyika Jana wilayani humo, Picha Mary Margwe.