December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shindano la KCB EAST AFRIKA GOLF TOUR laanza rasmi

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Shindano la Wazi la “KCB East Africa Golf Tour”limeanza Rasmi siku ya Leo katika Klabu ya Gofu ya ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari hii Leo Meja Jenerali Ibrahim Mhona Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo amesema,Lugalo Gofu imekuwa ikiwandaa Watoto kwaajili ya Timu ya Gofu Kwa Miaka ijayo na anaipongeza KCB Bank Kwa kuunga Mkono Juhudi hizo Kwa Kupitia shindano la “KCB East Africa Golf Tour”.

Kwa Upande wake Cosmas Kimario Mkurugenzi Mkuu wa KCB Tanzania amesema,Leo wamefungua rasmi shindano la “KCB East Africa Golf Tour “likiwa na lengo la kupata Wachezaji wanne watakao iwakilisha Tanzania Kwenye Fainali nchini Kenya Mwezi Disemba na Matarajio yake Wachezaji hao Wataibuka kidedea.

Naye Alli Kayombo Nahodha wa Timu ya Watoto (Juniors) Lugalo Gofu amesema,wanashukuru Kwa kupata Fursa ya kushiriki Shindano Hilo kwani inaongeza Chachu ya kukuza vipaji vyao katika Mchezo wa Gofu.

Shindano la “KCB East Africa Golf Tour” ni Shindano la siku Moja ambapo linatizamiwa kufungwa Leo katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam.