Na Penina Malundo, Timesmajira
SERIKALI imesema itaendelea kutumia sheria ya nyuki namba 15 ya mwaka 2002 kuwawajibisha na kuwadhibiti wafugaji na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki ikiwamo asali na nta wasiozingatia ubora kwa kuwa wanaharibu sifa za mazao hayo kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 19 ,2024 na Afisa Nyuki Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Felician Shayo kuelekea maadhimisho ya siku ya nyuki duniani baada ya ziara yao ya uwandani kwa wadau wa sekta ya nyuki katika Wilaya ya Dodoma na Chamwino .
Kadhalika Shayo amewataka wadau katika sekta hiyo wanaojishughulisha na uongezaji thamani wa mazao ya nyuki kuzingatia ubora ili kulinda heshima ya soko bidhaa hiyo la ndani na Nje.
Kwa upande Wake Meneja wa Kiwanda cha Swahili honey,Akram Issa amesisitiza kuwa ili kulinda soko la kimataifa wazalishaji wanapaswa kuzingatia ubora kuanzia ufugaji hadi uvunaji wa mazao yatokanayo na nyuki.
Ziara ya wadau hao uwandani ni sehemu ya maadhimisho ya siku nne kuelekea kilele cha siku ya Nyuki Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, imeshirikisha wafugaji na wajasiriamali kwa kutembelea viwanda vya uongezaji thamani wa mazao ya nyuki Ili kujiongezea maarifa yenye tija kwa ukuaji wa sekta ya nyuki nchini.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best