November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea udiwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughule (kulia) akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Samaki Feri na kuwaomba kuichagua CCM kwa nafasi ya udiwani, mbunge na urais.Picha zote na Heri Shaaban

Sharik aahidi kuleta maendeleo Kivukoni

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Dar es Salaam

MGOMBEA udiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sharik Choughule amesema akichaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Kivukoni katika uongozi wake miaka mitano ataleta maendeleo makubwa kuijenga kata hiyo kuwa ya kisasa.

Mgombea udiwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughule (kulia) akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Samaki Feri na kuwaomba kuichagua CCM kwa nafasi ya udiwani, mbunge na urais

Sharik ameyasema hayo Kata ya Kivukoni leo wakati wa akipita katika soko la samaki la Feri kuomba kura za Rais John Magufuli na mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa tiketi ya CCM.

“Mkinichagua kuwa diwani wa Kata hii nitaboresha miundombinu ya Soko la Samaki la Feri soko liwe la kisasa na kuongeza fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwemo kuvipatia vikundi vyote mikopo ya Serikali inayotolewa ngazi ya Halmashauri ya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ” amesema Sharik.

Mgombea udiwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughule (kulia wa kwanza) akimwandaa samaki katika soko la Samaki Feri leo wakati akiomba kura za za Rais John Magufuli na mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na udiwani.

Sharik amesema Kata ya Kivukoni imepata bahati kubwa sana ina kitega uchumi soko la kisasa hivyo kila mwananchi wa kata hiyo siku ya Oktoba 28/2020 apige kura ya udiwani kwa Sharik,ubunge Mussa Zungu na Rais wetu John Magufuli .

Amesema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa katika uongozi wake katika nchi yetu kuelekea Tanzania ya Viwanda ambapo kwa sasa tumefikia uchumi wa kati ameweza kuboresha miundo mbinu ya Reli ya kisasa,kununua ndege kujenga barabara kuboresha sekta ya afya nchi nzima.

Aidha amesema mambo mengine yaliofanya na Rais kuboresha soko la samaki feri ,Mkakati ya elimu bila malipo yote yamefanywa na John Magufuli sasa hivi watoto wetu wanasoma bila kulipa ada

Sharik amesema atashirikiana na wafanyabiashara wa soko la Kimataifa la Feri pamoja na Wafanya biashara wa soko hilo katika mambo mbalimbali kila wakati hivyo wasiwe na wasiwasi katika shughuli za uzalishaji na uvuvi wote waendelee kukiamini chama chao cha Mapinduzi CCM kwa maendeleo endelevu.

Amewakikishia kuwapatia mikopo ya Serikali wafanyabiashara wote wa Mama Lishe na Baba Lishe wa wanaofanya shughuli katika soko hilo wamchague kwa kishindo ili aweze kuwa diwani awasimamie mikopo hiyo ajili ya vikundi vyao.