Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Watanzania wametakiwa kutumia vizuri chakula ili kukabiliana na tishio la njaa linaloonyemelea afrika.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ametoa wito huo kwenye kikao na wanachama wa ccm wa kata ya Mdimba Wilaya ya Tandahimba mkoa wa Mtwara ambako yuko kwenye ziara ya siku nne.
“Ndugu zangu shirika la chakula duniani limetangaza tahadhari ya hali ya chakula duniani… kwahiyo naomba tuweke akiba ya chakula” alisema Shaka na kuongeza
“Nchi kadhaa zimetangaza hali ya hatari hao wanaoshughulika na chakula duniani(Wfp) wanasema watu zaidi ya milioni 80 Afrika wako kwenye hatari hiyo”
Amesema vita vya Ukraine vimechangia hali hiyo.” Mnasikia kwenye vyombo vya habari vita huko Ukraine vimesababisha upungufu wa ngano kwasababu asilimia takriban 40 ngano inatoka huko”
More Stories
Kapinga asema mafanikio katika sekta ya nishati yanatokana na jitihada za Rais Samia
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi