Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameiagiza Serikali ya Mkoa wa Mtwara kuacha urasimu kwa kuchelewesha ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wa korosho mkoa humo.
Shaka ametoa maagizo hayo baada ya kuwasili Mkoa wa Mtwara kwa ziara ya kikazi akitokea mkoani Lindi ambapo baada ya kufika Mtwara alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na miongoni mwa kero hizo ni baadhi ya vijiji kutopata pembejeo hali inayotia wasiwasi kwamba huenda itachelewesha maandalizi mikorosho kuelekea msimu mpya wa zao hilo.
“Tumetoka asubuhi tumezungumza na Mkuu wa Mkoa taarifa ambayo nimepatiwa pembejeo zimeshafika, hivyo niwatake Serikali ya Mkoa wa Mtwara waache urasimu, ndani ya wiki moja pembejeo ziwe zimetoka, tunataka wananchi wanufaike na uwepo wa Rais Samia ambaye ameamua kutoa bure pembejeo za kilimo, lengo kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao,” alisema Shaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Meja Jenerali Marko Gaguti, amesema amepokea maelekezo hayo na atakwenda kuyafanyia kazi huku akiahidi pembejeo hizo kuanza kuwanywa leo hii wilayani humo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba