December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikalini yaanza mapitio sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004

Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma.

OFISI ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu imeanza mchakato wa mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa watu wenye ulemavu ya 2004 ili kukidhi mahitaji ya sasa na baadae na kuzingatia malengo ya kijinsia.

Akizungumza katika kikao cha wadau wanaotekeleza mchakato huo jijini hapa leo,Agosti 24,2023,Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu ,Prof.Jamal Katundu ameeleza kuwa mapitio hayo yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake(UN Women).

Prof.Jamal amewataka wadau hao wanaotekeleza mchakato huo kuhakikisha uwakilishi wa makundi yote ya watu wenye  walemavu katika mchakato wa kupata maoni wanashikishwa.

“Ni wape mfano mmoja mimi sipandi usafiri wa umma ukija kuniuliza sasa hivi nauli kiasi gani sitajua ila ukimuuliza anayepanda usafiri huo anajua nauli kiasi gani,hivyo huko mnakoenda mmeniambia mtaenda kwenye halmashauri mtakutana na maafisa Elimu,maafisa ustawi wa jamii lakini hakikisheni mnakutana na walengwa wenyewe,”amesema Prof.Jamal.

Kwa upande wake Mshauri Elekezi katika mchakato huo ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)Dkt.Consolata Sulley amesema kuwa wamekutana wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na shirika la UN Women kwa kusrikiana wote ili kufanya mapitio ama tathmini ya sera ya maendeleo na huduma kwa watu wenye ulemavu iliyopitishwa mwaka 2004.

Amesema wameona kwamba kwa kushirikina na serikali kuna uhitaji wa kufanya tathmini na mapitio  ya sera hiyo kwasababu imechukuwa muda mrefu lakini pia wanataka kuona namna gani sera hiyo inazingatia masuala ya kijinsia kwa huduma ya maendeleo ya watu wenye ulemavu.

“Kwahiyo sasa tupo kwenye hatua za awali za kufanya mapitio hayo na katika mapitio hayo tutafanya utafiti kwani tutazungumza na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali yenyewe,serikali za mitaa pia tutaenda kwenye halmashauri na kule tutazungumza na watu lakini vilevile tutashirikisha wanufaika wenyewe ambao ni watu wenye ulemavu kupata maoni yaona kuweza kupata tathimini hiyo ambayo pia itatusaidia kufanya maboresho kupata sera ambayo itazingatia haki za watu wenye ulemavu lakini kwa kuzingatia pia jinsia wanawake na wanaume,”amesema Dkt.Sulley

Naye Mwakilishi wa UN Women, Jacob Kayombo amesema kuwa shirika hilo limepokea  fursa ya kufanya kazi na ofisi ya Waziri Mkuu  kwa heshima kubwa kwani wanafanyia kazi eneo ambalo tayari limeshafanyiwa kazi kubwa .

“Kama shirika la umoja wa mataifa ambalo limepewa adhima na serikali katika kushirikiana na jambo hili katika kuinua  na kuleta usawa kwa watu wenye ulemavu kupitia shughuli hii shirika linasema hatua tuliyofikia ni nzuri kwani tunaona ushirikiano mkubwa hivyo tutafikia malengo kwani hapa kila mtu anajihisi ni sehemu ya jamii hiyo hiyo ya watu wenye ulemavu,”alisema Kayombo.

Huku Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA)Jonas lubago ameishukuru serikali kwakutimiza ahadi yake kwani wao kama Shirikisho la watu wenye ulemavu walikuwa wanataka jambo hilo kwa muda mrefu na sasa limeanza kufanyiwa kazi.

“Ili jamboni ni kubwa sana kwetu na tulikuwa tunakuja kwenye ofisi yako kulitaka hili jambo na tunashukuru leo hili jambo kweli linaenda kutokea na mara nyingi tunapokuja kwenye ofisi yako tunasaidiwa zaidi ya tunavyotarajia tunshukuru sana.

“Hii ni chachu na kwachahu hii tunakuja na sera ambayo itatazama maisha yalioyopo katika jamii kwa ksasa lakini kwa baadae dunia inaendaje kuhusu hii sera,”amesema