Na Mwandishi wetu Timesmajira online
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amewatoa hofu na kuwahakikishia watuamiaji wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) kuwa zipo za kutosha na kuwataka kuacha kwenda kuzigombania katika vituo vya afya .
Msigwa ametoa kauli hiyo wakati akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Machi 1 ,2025 kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoifanya hivi karibuni Mkoani Tanga.
“Kuna baadhi ya watu wameanza kupata hofu na kupelekea kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupewa dawa za miaka miwili na kuendelea…ukichukua dawa ukienda kuziweka nyumbani zitaaribika na zikiaribika azitakusaidia bali zitakuletea shida katika afya ..acheni dawa zikae vituo vya afya zinapohifadhiwa vizuri huku nyinyi mkifuata utaratibu mnaopewa na wataalamu wa kwenda kupokea kama ambavyo utaratibu unavyosema”amesema Msigwa

Amesema watanzania wanapaswa kutambua kuwa dawa za ARV zipo za kutosha na tayari Serikali imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kununua kwa ajili ya kuwapatia ili waendelee kuishi.
“Nawaomba watanzania wanaotumia dawa za ARV kuishi kwa amani na kuendelee kuchapa kazi na kuchukua taadhari za kutosha na kutokuwaambukiza wengine dawa zipo Serikali yenu ipo inawaangalia na atutaishiwa wala amtakosa dawa”amesema
Aidha amewaomba vijana kuendelea kuchukua taadhari kwani ukimwi bado upo na kuwataka kujikinga .
“Dunia kwa sasa imekuwa ikizungumzia kumaliza kabisa ugonjwa wa Ukimwi hivyo watanzania tunapaswa kuwa wa kwanza kuumaliza na inawezekana kuyakata maambukizi ni raisi si mnaona tumepita kwenye CORONA tumeweza kupata uzoefu kama tumeweza kuvaa barakoa mtu uwezi kushidwa kuvaa ile nyingine”alisisitiza Msigwa
More Stories
UVCCM waonywa kuwa ‘machawa’
Wahifadhi Wanawake wa TAWA Watembelea Pori la Akiba Wami-mbiki
Halmashauri Rungwe yapongezwa nafasi ya kwanza matokeo kidato cha nne