Na Rose Itono- Morogoro
SERIKALI imeziagiza Bodi zenye Mamlaka ya Usimamizi katika Sekta ya Ujenzi kuhakikisha wataalamu wanaopewa dhamana ya kutekeleza miradi ya Ujenzi wanazingatia sheria za Kodi Ili serikali iweze kupata mapato na Shughuli za ujenzi ziendelee kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi
Akifungua mafunzo endelevu ya wataalamu wa Majenzi yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) mjini Morogoro jana Katibu Tawala Msaidizi,Miundombinu wa Mkoa huo Mhandisi Ezron Kilamhama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alisema katika baadhi ya miradi ya Ujenzi inayosimamiwa na kutekelezwa na wataalamu wa ndani ukwepaji wa kodi umekuwa mkubwa kiasi cha kusababisha malalamiko dhidi ya umahiri na ujuzi wa Kampuni za ndani
Alisema kaguzi ambaxo zimekuwa zikifanywa na mamlaka za Usimamizi kwenye miradi yetu zimekuwa na mapungufu makubwa kwenye ubora na gharama za miradi kuwa juu.
“Nimefurahia sana kusikia katika mafunzo haya kutakuwa na mada ya Mapitiio kuhusu uzingatiaji wa masuala ya kodi, mada hii itukumbushe uwajibikaji, ufuatiliaji na uzingatiaji wa nidhamu ya kulipa Kodi katika kuendeleza Sekta ya Ujenzi,” Amesisitiza Mhandisi Kilamhama
Ameongeza kuwa, kuhusu mada ya ulinganifu wa gharama za ushauri kwa mujibu wa sheria ya AQRB na ya PPRA mada hii itadaidia kupata uelewa wa pamoja Juu ya ukokotoaji wa ada za ushauri kwa kutumia sheria hizi mbili za AQRB na PPRA
Pia amesema kwenye mada ya Usimamizi wa miradi katika Tasnia ya Ujenzi Nchini Tanzania mada hii ni muhimu hasa wakati huu ambapo serikali na Sekta binafsi zinatekekeza miradi mingi ya Ujenzi ambayo imekuwa kichocheo Cha ukuaji wa uchumi Nchini
“Bila wataalamu wetu kusimania vyema miradi hii hatutaweza kupata matokeo yanayoendana na thamani ya uwekezaji unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi,”amesema Mhandisi Kilamhama
Akifafanua kuhusiana na
Changamoto mbalimbali zinazoikabiliwa na sekta hiyo ikiwemo ya baadhi ya Taasisi za umma zinavyotekekeza miradi ya Ujenzi kwa utaratibu wa kutumia wataalamu wa ndani ya Taasisi yaani ‘Force Accaunt’ isivyo sahihi serikali imeliona suala Hilo na kila mara viongozi wakuu wa serikali wamekuwa wakitolea maelekezo kuwa sheria ya ununuzi wa umma inayohutaji wataalamu watumike uzingatiwe
Amesema serikali itaendelea kushirikisha kikamilifu wataalamu wa ndani katika hatua zote za ujenzi katika miradi ya Ofisi za halmashauri na Manispaa,Majengo ya hospitali za Rufaa,Mkoa na Kanda pia masoko makubwa ya Kusasa na miradi ya Ujenzi wa vitui vikubwa vya mabasi ya masafa marefu unatekekezwa kwa kutumia wataalamu waliosajiliwa na bodi
Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya AQRB Mkadiriaji Majenzi Nyaswa Kalomo kwa niaba ya Msajili wa Bodi hiyo ameiomba Serikali kuendelea kuajiri wataalamu waliosajiliwa na bodi katika ofisi zote za umma Ili kutoa miongozo ya ujenzi kwa waendelezaji wa Majengo waliopo mjini na vijijini
Amesema idadi ndogo ya Wabunifu wa Majengo, wakadiriaji Majenzi, Wabunifu madhari na wataalamu wengine wa ujenzi unachangia kwa kiasi kikubwa taifa katika ushiriki wa miradi mbalimbali
“Kukosekana kwa sheria ya Majengo ,sheria hii Ina nanufaa mengi kwenye Tasnia ya Majengo sambamba na wataalamu kuhusika moja kwa moja kupanga,kubunu, kujenga na kutunza Majengo na mazingira kwa kuzingatia usalama na afya ya watu na Mali, kudhibiti ubora wa vifaa vya ujenzi matumizi Bora ya mifumo na miundombinu ya maji, gesi, nishati, mwanga, upepo, joto na baridi ndani na nje ya jengo pamoja na kutunza mazingira
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Ludigija Bulamile alisema mafunzo haya kwa wataalamu wa ujenzi ni muendelezo wa taratibu za Bodi ya AQRB katika kuwanoa wataalamu Ili kuwawezesha kupendana na mabadiliko ya teknolojia ya Ujenzi
“Uchaguzi wa mada umefanywa mahusus ili kuwakumbusha wataalamu wetu umuhimu wa kusimania miradi ya Majengo na mazingira katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku,”alisema Dkt Ludigija na kuongeza kuwa mada kuu ya mafunzo hayo ni Usimamizi wa Miradi katika Tasnia ya Ujenzi Tanzania ambayo utajadiliwa pamoja na mada ndogo zingine nne
Hata hivyo amezitaja mada zingine zitakazojadiliwa kwenye mafunzo hayo kuwa ni pamoja na ushughulikiaji wa madai na masuluhisho ya migogoro katika Tasnia ya Ujenzi nchini,mapitiio kuhusu uzingatiaji wa masuala ya Kodi na ulinganifu wa gharama za ushauri kwa mujibu wa sheria ya AQRB na PPRA
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu