November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yawataka wasomi kutofungia elimu na tafiti zao ndani

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Serikali imewataka Waitimu Wa vyuo mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa hawafungii matokeo ya Tafiti zao na badala yake watumie matokeo ya Tafiti lakini pia elimu zao Katika kuleta matokeo chanya ndani ya Jamii.

Endapo kama kila muhitimu wa ngazi mbalimbali ya elimu ataweza kutumia ipasavyo ujuzi alioupata itaweza kuiraisishia Jamii kuepukana na changamoto mbalimbali.

Hayo yameelezwa Arusha na Naibu waziri wa kilimo David Silinde Wakati akiwatunuku vyeti wahitimu kutoka katika chuo cha uasibu Arusha kwenye maafali ya 25 ambayo yalifanyika katika hoteli ya Ngurdoto.

Waziri Silinde alisema kuwa matokeo ambayo yanatolewa na watafiti ambao wameitimu vyuo vikuu ni mazuri Kwa kuwa yanakuja Kabisa na Majibu hasa Yale ambayo yanaikabili Jamii.

“nawasihi sana wasomi hakikisheni kuwa hamhifadhi Elimu ambazo mmezipata na badala yake njooni na majibu juu ya changamoto mbalimbali ambazo bado zinaitesa jamii yetu ya kitanzania toeni Majibu Kwa Serikali Lakini pia hata Kwa sekta bonsai “aliongeza.

Wakati huo huo alizitaka taasisi Za elimu hapa nchini kuhakikisha kuwa zinaendelea kutoa, elimu bora Kwa watanzania ikiwa ni utekelezaji Wa malengo ya Milenia.

Katika hatua nyingine mkuu wa chuo hicho cha Uasibu Arusha Profesa Eliamani Sodeyeka alisema Kwa kuzingatia maitaji mbalimbali Ndani ya jamii chuo kimeendelea kufanya Tafiti ambazo zinalenga kuja na majibu chanya Kwenye Jamii.

Profesa Sodeyeka alisema wanatarajia kuanzisha mitaala ya kilimo-biashara, ufugaji Lakini pia ufundi na utalii katika kampasi Za Babati pamoja na Songwe.

Alifafanua kuwa lengo la kuanzishwa Kia Mitaala hiyo ni kuwa Ndani ya maeneo hayo kuna watu ambao wanajituma zaidi katika Kazi lakini pia wanajishugulisha na kilimo, ufugaji na utalii.

Aliongeza kuwa kuanzishwa Kwa mitaala hiyo itaweza kusaidia jamii kupata elimu,ujuzi,na maarifa ya namna ya kuboresha shuguli zao.

Alihitimisha Kwa kusema kuwa Tanzania bado inahitaji Wasomi walio na nidhamu,uzalendo, maadlili mema ambao wanatumia maarifa,ujuzi,katika kuwatumikia watanzania Kutatua changamoto zinazoikabili Jamii.