November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yatoa maagizo TRA

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

SERIKALI imeitaka MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA kuwatambua na Kutoa motisha Kwa Wafanyabiashara wanayofanya vizuri katika mashirikiano ya kulipa Kodi ikiwa ni pamoja na kuwapa vyeti na zawadi mbalimbali.

Aidha Aliipongeza TRA Kwa kutumia mbinu rafiki za kukusanya mapato ambazo zimeipa ushirikiano mkubwa kati yao na walipa kodi nchini Huku akibainisha kuwa mahusiano Yao yakuwa yenye tija na mafanikio iwapo TRA itatanguliza weledi na ufanisi katika shughuli zake za ukusanyaji wa mapato

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Naibu waziri wa fedha kutoka wizara ya fedha Hamad Chande wakati wa kilele Cha kufunga wiki ya kuhamasisha matumizi sahihi ya EFD Kwa kudai na kutoa risiti, ambapo aljsema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua Kali na za haraka pale ambapo itabaini hakuna matumizi sahihi ya mashine za EFD Kwa Wafanyabiashara kutokana na kitendo hicho kuwa kinyume na sheria.

“Nawapongeza watumishi wetu wa TRA tofauti miaka ya nyuma na ya leo , miaka ya nyuma mtumishi wa TRA akikusanya mapato alikua anaonekana adui sana kwasababu alikua anatumia mbinu ambazo siyo rafiki, lakini sasa mnatumia mbinu rafiki hivyo nawapongeza sana”

“Hili ndiyo pekee linatupelekea kujenga Taifa hili, yaani mlipa Kodi analipa Kodi kwa wakati na hiari na na mkusanyaji Kodi anaenda kirafikk na upendo, hili linawezekana kabisa ikiwa mahusiano ya watumishi wa mamlaka na wafanyabiashara yatakua yenye tija na mafanikio yanayotanguliza uweledi, iwajibikaji, maadili, na uhusiano mwema unaojengeka kupitia matukio mbalimbali kama haya ya michezo, bonanza na watumishi kutembelea maeneo yenu ya biashara kirafiki zaidi”

Hata hivyo amewataka Wafanyabiashara WA soko la kariakoo kuwa mstari wa mbele kulifanya soko la kariakoo kuwa soko la kimataifa Kwa maslahi mapana ya uchumi wa nchi na Wafanyabiashara Kwa ujumla Huku akiwasisitiza Kutoa risiti sahihi pindi wanapofanya mauzo Kwa kutumia mashine za EFD ili kuepuka udanganyifu.

“Mchango wetu watu wa kariakoo na Ilala ni mkubwa sana katika kuendeleza biashara pia kukuza uchumi wa Taifa letu, ushiriki wenu huu siku ya leo inamaana mnatambua kuwa kwa pamoja tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kulifanya kariakoo kuwa soko la Kimataifa “

“Mashine za EFD Zina jukumu muhimu kusimamia ukusanyaji wa mapato, na kuhakikisha uwazi na nadhamu katika mifumo ya kifedha ya nchi yetu, hivyo tutoe risiti sahihi kwa wale wanaouza na wale wanaonunua Wadai risiti”

Naye Kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Alphayo Kidata amewataka Wafanyabiashara nchini kuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu zazo za biashara ili waweze kuzitumia kufanya ulinganifu na kuepuka migogoro pindi maafisa ukaguzi kutoka TRA wanapopita katika maeneo Yao ya Biashara.

Aidha amesisitiza elimu ya mlipa Kodi iendelee kutolewa kwani wafanyabiashara wanaongezeka Kila siku nchini.

“Tutaendelea kueleimishana wenyewe kama wenyewe na kuwa Mabalozi kwa wengine katika ukusanyaji kodi”

Nao badhi ya washiriki walioshiriki katika wiki hiyo akiwemo Meneja wa kampuni ya SOFTEN technologies amabao ni wasambazaji wa mashine za EFD, Salim Kambangwa amewataka Wafanyabiashara kutambua kwamba utoaji wa risiti ni kitu kizuri na waachane na dhana potofu ya kwamba mashine inakata asilimia 18 pindi wanapotoa risiti.

Wiki ya kuhimiza matumizi sahihi ya EFD Kwa Kutoa na kudai risiti ilianza rasmi September 23 mwaka huu na kuhitimishwa juzi.