Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
SERIKALI ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha sh bil 24.6 kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji uwanja wa ndege Tabora ambapo jengo jipya la abiria la ghorofa mbili limeanza kujengwa.
Akizungumza baada ya kutembelea uwanja huo juzi, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia kiasi hicho cha fedha ili kuufanyia maboresho makubwa uwanja huo.
Amebainisha kuwa mradi huo ambao umeanza kutekelezwa mwaka jana unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hivyo kuwezesha ndege nyingi na kubwa kutua katika uwanja huo na kupatikana huduma muhimu zote.
‘Mkandarasi alitakiwa kumaliza kazi hii mwezi Machi 2024 lakini ameomba kuongezewa muda zaidi kutokana na vifaa vilivyoagizwa kutoka nchini India na China kuchelewa kufika’, alisema.
Profesa Mbarawa amemwagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kuhakikisha vifaa vyote vilivyoagizwa kutoka nje vinafika kwa wakati ili mradi usichelewe.
Amebainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawezesha huduma za usafiri wa anga kupatikana kila siku na kuongeza kuwa uwanja huo utakuwa na mwonekano wa kisasa kwa kuwa na njia 2 za kurukia ndege na kifaa cha kuongozea ndege.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani hapa Mhandisi Raphael Mlimaji ameeleza kuwa mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya utekelezaji wake umefikia asilimia 23.
Ametaja faida za mradi huo kwa wakazi wa Tabora kuwa ni kuwarahisishia usafiri wa anga, kusaidia shughuli za kibiashara, kuwarahisishia shughuli za kijamii, kusaidia shughuli za utafiti na kilimo, kukuza utalii na kukuza uchumi wa Mkoa.
‘Mheshimiwa Waziri tunakuhakikishia kuwa tutasimamia ipasavyo utekelezaji mradi huu ili thamani ya fedha iendane na kazi iliyofanyika na ukamilike kwa wakati’, amesema.
Naye Mkuu wa Mkoa Balozi Dkt Batilda Burian ameeleza kuwa mradi huo utaufanya Mkoa huo kuwa kitovu cha uchukuzi na shughuli mbalimbali za usafirishaji bidhaa na mazao ya wakulima zitafanyika.
Amebainisha kuwa mradi huo umewezesha vijana wazawa wa kike na kiume kupata ajira na kuongeza kuwa watafuatilia kwa ukaribu zaidi utekelezaji wake ili ukamilike haraka na kwa viwango vinavyotakiwa.
Meneja wa Uwanja huo Fadhil John amesema kuwa mradi huo una manufaa makubwa kwa wakazi wa Mkoa huo kwani utawezesha abiria 60 kukaa kwa wakati mmoja.
Faida nyingine ni uhakika wa usafiri wa ndege kila siku ikiwemo kuongeza idadi ya ndege zitakazokuja Tabora, kuongeza wawekezaji, kurahisisha shughuli za kibiashara kwa kuwa bidhaa za Kitanzania zitauzwa uwanjani hapo,
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba