Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MKURUGENZI wa Idara ya Huduma za Kisheria,kutoka Tume ya Haki za Binadamu,Nabor Assey amesema Serikali inatambua wajibu wa Azaki za kiraia katika mchakato mzima wa tathimini yakutoa mapendekezo ya haki za Binadamu nchini Tanzania.
Akizungumza juzi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika mjini Morogoro umewakutanisha wadau takribani 40 kutoka katika Asasi za kiraia,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Wizara ya Katiba na Sheria, Assey amesema Serikali ipo pamoja na wa watu wa azaki katika mchakato huo kwa lengo la kuhakikisha mapendekezo yanayotolewa yanakubalika.
“Kwa niaba yenu tunaishukuru Serikali katika kutekeleza mapendekezo hayo kwani takribani mapendekezo 187 tayari yamekubalika juu ya masuala ya haki za binadamu,”amesema na kuongeza
“Kama asasi za kiraia zinapaswa kuwa mstari wa mbele kuleta matokeo chanya katika maeneo ambayo yamekubalika kufanyiwa kazi ,”amesema
Kwa Upande wake Afisa Uchechemuzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC)Nuru Maro , amesema Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini umeendesha kikao kazi cha wadau wa Asasi za Kiraia cha kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyokubaliwa na serikali katika mchakato wa mapitio ya hali ya haki za binadamu (UPR).
Amesema katika Kikao hicho wadau hao waliweza kupitia mapendekezo yaliyokubaliwa na serikali katika mchakato wa UPR na pia kujadili mapendekezo yaliyokataliwa na kuona namna watakavyoweza kufanya uchechemuzi ili mapendekezo hayo yaweze kukubliwa na kufanyiwa kazi.
“UPR ni mchakato unaoendeshwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhakiki hali ya haki za binadamu kwa nchi zote ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa lengo kuu la utaratibu huu ni kuboresha hali ya Haki za Binadamu katika nchi zote na kushughulikia ukiukwaji wa haki za binadamu ili kuifanya dunia sehemu salama kwa kila binadamu,”amesema na kuongeza
“Mwaka 2021, Tanzania ilifanyiwa mapitio ya tatu ya hali ya haki za binadamu (UPR) mnamo tarehe 05 Novemba 2021 katika mkutano wa 39 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Tanzania ikiwakilishwa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, ilipokea jumla ya mapendekezo 252 kutoka nchi mbalimbali. Katika taarifa ya wali, mapendekezo 108 kati ya 252 sawa na asilimia 43 yalikubaliwa, 12 sawa na asilimia 4.8 yaliahirishwa kwaajili ya kufanyiwa maamuzi na mapendekezo 132 sawa na asilimia 52 hayakukubaliwa, “amesema
Kwa Upande wake, Ofisa Praogramu wa THRDC,Perpetua Senkoro amesema Kutokana na asilimia ya mapendekezo yaliyokubaliwa kupungua kutoka asilimia 70 kwa mwaka 2011,asilimia 58 mwaka 2016 na kufikia asilimia 43 kwa mwaka 2021.
” THRDC kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Save the Children iliratibu mkutano wa wadau kutoka asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu kwa kusudi la kupitia mapendekezo yote 252 na kuishawishi serikali kukubali mapendekezo zaidi.
THRDC inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusikiliza maoni ya wadau na kuongeza idadi ya mapendekezo yaliyokubaliwa kama ilivyoainishwa katika nyongeza ya ripoti ya nchi ya tarehe 21 Machi 2022. Katika nyongeza hii, idadi ya mapendekezo yaliyokubaliwa imeongezeka maradufu toka 108 yaliyokubaliwa awali hadi 187 yaliyokubaliwa kwenye ripoti ya mwisho, (20 kati ya hayo yakikubaliwa kwa sehemu).
Hii imepelekea idadi ya mapendekezo yaliyokataliwa kupungua toka 132 kwa awali hadi 65 kwa sasa.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi