January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yataka wazazi wachangie chakula shuleni

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala


Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila, amewataka Wazazi wote katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangia pesa ya chakula shuleni Ili mtoto aweze kupata mlo na kupelekea kufanya vizuri katika masomo yake.

Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, amesema hayo wilayani Ilala wakati wa kupokea msaada wa Madawati 200 kutoka Benki ya !(NMB) ambapo madatawati hayo yamegaiwa kwa shule za msingi zlizopo Wilaya ya Ilala .

” Nawapongeza Benki ya NMB kwa msaada wenu na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es asalaam katika kusimamia sekta ya Elimu naagiza katika Mkoa wangu wa Dar es Salaam kitu cha Msingi kwa Watoto chakula mzazi kuchangia shuleni sio mchango shuleni ni agizo la lazima mtoto apate mlo aweze kufanya vizuri darasani kitaaluma ” amesema Chalamila .

Mkuu wa Mkoa Chalamila amesema kampeni ya chakula shuleni ni lazima sio ombi vitu vingine vya lazima mavazi na malazi ni lazima sio mchango kwa mwanafunzi .

Amesema masuala ya Afya ya mtoto ni jukumu la Wazazi mtoto apate Afya njema aweze kusoma vizuri Taifa letu liweze kupata viongozi bora wa kesho.

Aliwataka wazazi kushirikiana na Walimu katika sekta ya Elimu watoto waweze kupata Mazingira shuleni na kukemea vitendo vya momonyoko wa maadili .

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipongeza Benki ya NMB kwa ushirikiano wao katika kukuza Elimu wamepokea msaada wote wa Madawati yenye thamani ya shilingi milioni 51 Madawati hayo yataelekezwa katika shule zote .

Mkuu wa Wilaya Mpogolo amesema Wilaya ya Ilala ina shule 131 za Msingi na Shule za Sekondari 93 wamepokea bilioni 9 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari za madarasa

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema mabucha ya nyama ya Vingunguti wilayani Ilala yaliojengwa na Serikali wametoa ajira kwa Vijana 2000 .

Akizungumzia shule ya kombo amesema shule hiyo ina Wanafunzi 4000 Kata ya Vingunguti Jamii ya eneo hilo kila siku wazazi wanazaa watoto hivyo kuwa na ongezeko la watu wengi wanaipongeza Serikali imejenga shule ya Msingi Mnyamani watoto wa Buguruni Mnyamani waliokuwa wanasoma Vingunguti sasa hivi watasoma katika shule yao na kupunguza ongezeko la wanafunzi kusoma mbali .

Meya Kumbilamoto alipongeza benki ya NMB ni benki ya kwanza kuisaidia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika sekta ya Elimu na ina mpango wa kujenga vyoo Vingunguti