Na Tiganya Vincent,TimesMajira Online. Tabora
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ameutaka uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kusimamia zoezi la wavamizi wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima iliyopo wilayani Kaliua, wanaondoa mazao yao ambayo yamekomaa.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha TAWA, inaendesha shughuli zake za uhifadhi wa mazingira na wanyapori bila kikwazo chochote.
Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Wachawaseme kilichopo Isawima wilayani Kaliua alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Amesema uhifadhi ni muhimu na wenye manufaa makubwa ya taifa na wananchi kwa sasa na vizazi vijacho na hivyo serikali, haiwezi kuacha watu wavamie na kuharibu maeneo hayo.
Mary amesema kutokana na uamuzi huo wa wakulima, walivamia eneo hilo wanatakiwa kuondoa mazao yao kwa utaratibu maalumu, utakaopangwa na serikali kupitia vibali ambavyo vitabainisha nini mkulima alichonacho kwenye hifadhi hiyo, ili kuweza kutambua nani ni nani anaingia kenye hifadhi muda husika.
Amesema serikali haiwezi kuona watu wanavamia hifadhi zilizohifadhi kisheria na kuharibu miundombinu yake kwa sababu ya maslahi ya watu wachache na kuharibu manufaa ya watu wengi nchini.
Naibu Waziri huyo ameingiza Serikali ya Mkoa na TAWA, kuhakikisha watakapokamilisha zoezi la kuondoa mazao yao kwenye hifadhi hakuna mtu yeyote anayeingia ndani ya hifadhi kwa ajili ya shughuli zozote ya kibinadamu zinakinzana na uhifadhi.
Amesema kwa kufanya hivyo, kutasaidia hifadhi hiyo kuendelezwa kwa mshoroba wa wanyama na maji kuendelea kutiririka hadi Ziwa Tanganyika kwa asilimia 30.
Hata hivyo ameahidi kutuma wataalumu wa kupima mipaka kwa ajili ya kuelimisha wananchi wa vijiji 11 vilivyomo kwenye eneo la Isawima, ili kutambua mipaka yote ya kila kijiji na mwisho wa eneo ambalo wananchi hawapaswi kuingia wala kufanya shughuli za kibinadamu.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kamati ya Ardhi na Maliasilia na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Aloyce Kwezi amemweleza Naibu Waziri huyo kwamba wananchi wa eneo la Isawima ambalo eneo lake kubwa ni hifadhi wanaomba kutambua mikapa yake eneo lao.
Amesema kutokutambua mipaka hiyo, kumesababisha baadhi wa wananchi kuingia eneo la hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Philemon Sengati amesema uongozi wa mkoa hauwezi kuona watu wachache wanatumia fedha zao na kuingia katika eneo hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibindamu.
Amesema eneo hilo ni muhimu kuhifadhiwa kwa kuwa ni chujio la maji yanayoelekea Ziwa Tanganyika ni mazalia ya nzige wekundu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba