January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yasisitiza upatikanaji wa walimu bora

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema ili kupambana na ujinga ni muhimu kuwa na walimu bora ambao watapatikana katika mazingira bora na kutoka na stadi bora za kufundishia.

ADkt. kwilapo ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa siku mbili uliokutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha Mafunzo ya Ualimu nchini(TESP) ambao unafadhiliwa na Seriakali ya Canada

Amesema Tanzania kuna maadui watatu ambao ni umasikini na maradhi na ujinga, hivyo ili kuondoa matatizo hayo upo umuhimu wa walimu kutoka katika mazingira bora na hatimaye kupata stadi nzuri kufundishia.

Dkt Akwilapo amesema katika mradi wa TESP ambao ni wa miaka mitano umelenga zaidi kuboresha eneo la mafunzo ya uualimu tangu nchi hii ipate Uhuru ambapo jumla ya dola za Canada million 53 sawa na F sh. Billioni 84.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki katika mkutano wa siku mbili uliokutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha mafunzo ya ualimu nchini TESP ambao unafadhiliwa na Seriakali ya Canada picha na Mpiga. Na mpigab picha wetu.

“Madhumuni ya mradi huu ni kuimarisha ufundishaji kwa ujumla wake katika vyuo vya Ualimu ili kumuwezesha mwalimu kupata mbinu mbalimbali za kufundishia sambamba na kutengeneza miundombinu ya vyuo 35 ya Serikali na kufanyiwa maboresho mbalimbali kulingana na mahitaji kila chuo,”amesema Dkt Akwilapo

Vilevile amesema kupitia mradi huo vipo vyuo ambavyo vimejegewa maktaba sita ambavyo ni pamoja na chuo cha Tukuyu, Dakawa, Morogoro, Butimba , Mpwampwa pamoja na Kasulu.

Aidha amesema mbali na ukarabati pia mradi huo unatoa Mafunzo kwa wakufuzi kazini na kutoa vifaa vya kufundishia vya Tehama na kufundisha masomo ya Sayansi.

“Mafanikio ya mradi huu ni makubwa sana kwani hadi sasa tumefanikiwa kujenga chuo kipya cha kabanga ambacho muda sio mrefu kinakwenda kuzinduliwa,”amesema Dkt Akwilapo

Amebainisha kuwa mradi huo unatarajia kukamilika baada ya miaka miwili na malengo zaidi baada ya kukamilika ni kutoa walimu wenye sifa zinazotokana na stadi bora za kufundishia.

Naye mwakilishi kutoka Serikali ya Canada, Hellen Fytche amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuleta miradi mbalimbali ambayo italeta maendeleo chanya.

Aidha ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Ufundi, utawala wa maendeleo na vyuo vya uhalimu kufikiria njia nyingine kama mradi huo zenye kuleta tija katika miaka ijayo.