Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
SERIKALI imepiga marufuku uingizaji wa Majokofu ya Mtumba pamoja na viyoyonzi ambavyo vinatumia Gesi vimekuwa na madhara ya uharibifu wa tabaka la ozoni ambalo limekuwa na athari kwa afya za wananchi ikiwemo mabadiliko ya taba nchi.
Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo Septemba 13,2023 na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Dkt.Selemani Jafo wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya siku ya kimataifa ya uhifadhi wa tabaka la ozoni kuhusu kemikali zinazomomonyoa tabaka la ozoni ambayo yatafanyika Septemba 16 Mwaka huu.
Dkt. Jafo amesema tabaka la ozoni linapoharibiwa husababisha saratani ya ngozi, mtoto wa jicho, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi, kujikunja kwa ngozi, kuathirika kwa ukuaji wa mimea pamoja na kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo, alitoa wito kwa wananchi kununua bidhaa zilizowekwa nembo rasmi isemayo “Ozone friendly” au “low global warming potential” au yaani “sahibu wa Ozoni” au “uwezo mdogo wa kuchangia ongezeko la joto duniani”.
Pia ametaja madhara mengine kuwa ni kuathirika kwa ukuaji wa mimea vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
“Ukiangalia mwaka juzi (2021) kuna kazi mbalimbali zilikuwa zikifanyika kwa mafundi wa majokofu pamoja na kutembelea maduka ili kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa mafundi ili waweze kutambua madhara yake na kuchukua hatua,”amesema Jafo.
Mafunzo hayo yalilenga namna ya kudhibiti uingizaji wa kemikali nchini kwa Maafisa wa Idara za Serikali zilizopo katika Mpaka wa Namanga na kutoa elimu kwa wanafunzi wa fani ya viyoyozi katika Chuo cha Ufundi Arusha pamoja na mafundi wa viyoyozi na majokofu kwa mkoa wa Arusha kuhusu namna bora ya kukarabati vifaa hivyo pasipo kuachia angani kemikali na hivyo kuharibu mazingira.
Katika hatua nyingine,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya mabadiliko ya tabianchi Duniani kutokana na kujipambanua katika miradi mbalimbali kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Maadhimisho ya siku ya uhifadhi wa tabaka la ozni yanaenda sambamba na Kaulimbiu isemayo itifaki ya Montlio hifadhi ya tabaka la ozoni na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba