Na Heckton Chuwa,TimesMajira Online. Moshi
SERIKALI imesema haitawavumilia viongozi wa taasisi zake, au wale wa vyama vya ushirika ambao watatumia nafasi zao kuhujumu mali za umma.
Tahadhari hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa hafla ya kurudisha magari mawili mali za kiwanda cha kukobolea kahawa (TCCCo), kilichoko Moshi mkoani Kilimanjaro.
Magari hayo ni sehemu ya mali zilizouzwa kinyume cha taratibu ambapo uamuzi huo, umechukuliwa na serikali baada ya kikosi kazi kilichoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili kuchunguza kuuzwa kwa mali za TCCCo kubaini taratibu zilizokiukwa.
“Kuna waliopewa dhamana ya uongozi, aidha serikalini au kwenye vyama vya ushirika ambao wanatumia nafasi walizoaminiwa kuhujumu mali za umma kwa lengo la kujinufaisha binafsi, hawa serikali haitawavumilia pale watakapobainika,” ameonya Kusaya.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ