November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaombwa kukaa na wasambazaji wa kemikali za uchenjuaji dhahabu kufanya mazungumzo

Na David John

MKURUGENZI wa Kampuni ya Mayengo Traders LMTD inayojihusisha na usambazaji wa kemikali za kuchenjua dhahabu,Simon Mayengo ametoa rai Kwa Waziri wa Madini Dotto Biteko kuona umuhimu wa kukutana na wasambazaji wa kemikali hizo pamoja na wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza bidhaa hizo nchini pamoja na wachimbaji ili kuweza kuzungumzia changamoto zinazojitokeza wakati wanaingia bidhaa hizo nchini.

Amesema sababu za kukutana na makundi hayo nikuwaomba wauzaji wakubwa kuweza kuuza bei rafiki kemikali hizo Kwa wasambazaji ili na wao kama wasambazaji waweze kuuza bei rafiki Kwa wachimbaji wa Madini ya dhahabu hasa wachimbaji wadogo ili Kwa pamoja waweze kutengeneza mzunguko wa pesa na kiuchumi.

Mayengo ametoa wito huo leo ofisini kwake mbele ya waandishi wa Habari waliofika ofisini hapo Kwa lengo la kujua changamoto zinazowapelekea wao kama wasambazaji kuuza kemikali hizo Kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi inayotolewa na Serikali ya kuanzia shilingi laki 400000 hadi laki 600000.

Amesema kuwa biashara ya kemikali hiyo waliyowengi wanategemea hasa wachimbaji wadogo wanapofikia wakati wa kuozesha mchanga wanakuwa wameishiwa pesa, ya kununulia dawa hizo na kinachofanyika wao kama wachimbaji wanakuwa wanawahusisha watu wanaowauzia dhahabu Kwa maana ya (Madila).

Mkurugenzi wa Mayengo Traders Lmt.Simon Mayengo akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) .kuhusu upandaji wa chemikali za kuchenjua dhahabu.

Amefafanua kuwa Madila hao ndio wanakwenda kwao kama wasambazaji na kuwanunulia dawa wachimbaji ili waweze kwenda kumalizia shughuli zao ili mwisho wa siku iweze kupatikana dhahabu hivyo ushauri wao wanamuomba Waziri Biteko akutane na wafanya biashara wakubwa pamoja na wao kama wasambazaji ili Kwa pamoja waweze kutengeneza uchumi jumuishi .

“Tunamuomba Waziri Biteko akutane na hawa majayanti na sisi kama wasambazaji pamoja na wachimbaji wadogo kwani mara nyingi amekuwa akiwa tetea watu wachini pasipo kuangalia kama hapa chini biashara hii inafanyika vipi hivyo nitumie fursa hii kuwaambia wachimbaji wadogo ambao tunafanya kazi pamoja kwamba Mayengo General campan Traders limited iliyopo kahama. ipo “kwa ajili yao amesema

Nakuongeza kuwa ” Tupo Masumbwe na biadhaa zetu ni nafuu sana na tunauza Kwa bei nzuri sana Kwa kuanzia shilingi laki 600000 na shilingi laki 610000 hivyo wadau wa sekta ya dhahabu hasa wachimbaji wajitokeze kwenye magodauni yake kuweza kupata malighafi hizo na tuna kaboni aina tatu ambapo kaboni zote ni nzuri sana.” Amesisitiza

Mayengo ameongeza kuwa kaboni zilizopo ofisini kwake zinauwezo wa kuchoma dhahabu zaidi ya mara nne na hizo zinapatikana Mayengo tu na wao ndio mawakala ambao wapo kahama na wanauza Kwa bei nzuri ya shilingi laki 30000 Kwa maana kaboni ya kuchoma dhahabu hata mara nne .

Wakati huohuo akizungumzia zaidi biashara hiyo ya kemikali amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa Kwa watanzania kuchapa kazi na hakuna shaka kwamba Kanda ya ziwa dhahabu ndio tegemeo lao kubwa.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita Kwa kuweka udhibiti mkubwa kwenye sekta hiyo ya dhahabu kwani hivi sasa hakuna wizi wa dhahabu na Kodi ya Serikali inalipwa pasipo buguza ya aina yeyote hivyo anamshukuru Rais Dkt Samia Kwa fursa anayoitengeneza Kwa watanzania na wananufaika kupitia mazingira mazuri ya biashara.