Na mwandishi wetu, TimesMajira Online, Katavi
Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan lakumtaka Waziri mwenye dhamana ya Ardhi Jerry Silaa kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa Mtaa wa Rungwa Kata ya Kazima Mpanda Katavi na Chuo cha Kilimo Katavi (KUA) limefikia tamati baada ya Waziri wa Ardhi Jerry Silaa kukabidhi hatimilki za ardhi kwa wananchi hao.
Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi hatimilki za ardhi kwa wananchi hao Waziri Jerry Silaa alisema amefanikiwa kumaliza mgogoro huo kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Daniel Chongolo kwa Rais Samia Suluhu Hassan alipohitimisha ziara yake Mkoani Katavi, hivyo Rais kutoa agizo la kukamaliza mgogoro huo.
Waziri Silaa amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuagiza kumaliza mgogoro huu kuisha kabisa baada ya kuwa amepata taarifa kutoka kwa viongozi wa mkoa na Chama na kuongeza kuwa alimtaka kuhakikisha mwaka mpya ujao unaanza bila ya kuwa na mgogoro wowote.
‘’Nilikuja hapa tarehe 7 mwezi wa kumi mwaka huu na kutoa maagizo kwa Wizara ya Ardhi kuhakikisha inatekeleza maagizo ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwamba mgogoro huu ufike mwisho na niwambie tangu nipate uteuzi na kupewa maelekezo ya nini kifanyike sijawai kukutana na mgogoro wa ardhi ambao hautatuliki.’’Alisema Jerry Silaa Waziri wa Ardhi.
Katika hatua nyingine Waziri Silaa ameagiza Uongozi wa Mkoa wa Katavi pamoja na wananchi kitongoji cha Rungwa kuhakikisha wanalinda maeneo 13 ya wazi,hospitali, masoko,makabuli na maeneo ya shule za awali pamoja na shule za msingi na sekondari.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Iddi Kimanta amebainisha kuwa kuna viongozi wengi mkoani Katavi ambao kwa kipindi kirefu waliangaika na mgogoro huu bila mafanikio lakini jana Waziri mwenye dhamana ya ardhi alifanikiwa kumaliza mgogoro huo.
Kufuatilia hali hiyo Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Katavi alimtaja Waziri mwenye dhamana ya Ardhi Jerry Silaa kuwa anaingia kwenye historia kwa kufanikiwa kumaliza mgogoro huo.
Bw. Iddi Kimanta aliongeza kuwa taarifa za Chama na Serikali wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama mkoani Katavi taarifa zote zilitaja mgogoro huu na katika taarifa zote hizo walimuomba kuhakikisha anakomesha mgogoro huo ambao ulikuwa na maslahi mapana ya wananchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Jamila Yusufu amehaidi kuwa, kwa kuwa mgogoro huu umekwisha basi hawatakubali kuona unazalisha mgogoro mwingine kwenye neo hili maarufu KUA.
Tutasimamia kikamilifu, tutasimamia sheria kikamilifu,kuhakikisha eneo hili halizalishi migogoro ten ana niwaombe wananchi shukrani pekee ambayo tunaweza kumpa Mhe. Rais ni kutozalisha mgogoro mwingine katika eneo hili tena.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa