November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaipongeza OSHA kwa kazi zinazofanywa

Na Bakari Lulela,Timesmajira

SERIKALI imepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na mashirika katika kutetea na kuenzi shughuli za kibinadamu zinazofanywa kwa kuzingatia usawa na haki katika nchi yetu .

Akizungumza katika maadhimisho ya uzinduzi wa kumbukizi ya maafa yaliyowapata ndugu ZETU ambapo yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Edward Mpogolo aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

“Leo ni siku ya kuwakumbuka mashujaa wetu ambao walihangaika kwa ajili ya wengine, ambapo walijitolea kupitia nafasi zao nguvu zao, na hata maisha yao kwa ajili ya wengine Mpogolo amesema.

Aidha Mpogolo amesema katika maadhimisho hayo yalilenga zaidi kumbukizi na kuwapa ari wale wote wanaojitoa katika harakati za kuwapigania binadamu wengine kwa hali na Mali ikiwemo OSHA, save the children, Red cross, Zimamoto na damu salama.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano kutoka Wakala wa salama na Afya mahala pa kazi OSHA, Eleuter Mbilinyi amesema wao kama Wakala wa usalama na Afya mahala pa kazi wanashirikiana na wadau wengine katika utoaji wa elimu ya maafa na kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama .

Hivyo OSHA hushiriki katika kuwatengenezea wafanyakazi mazingira Bora na salama na kutambua umuhimu  wao katika kujenga uchumi wa nchi , vilevile kufanya kazi kwenye mazingira mazuri,pia vifaa na utekelezaji wa ufanyaji wao kuhakikisha una kuwa wenye weredi mkubwa.