November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaipongeza CBE kwa program atamizi na ya uanagenzi

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, akizungumza kwenye mahafali ya 58 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Sehemu ya wahitimu 1,226 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakiwa kwenye mahafali hayo ya 58 ya chuo hicho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wahitimu 1,226 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakiwa kwenye mahafali hayo ya 58 ya chuo hicho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wahitimu 1,226 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakiwa kwenye mahafali hayo ya 58 ya chuo hicho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, amewataka wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE kutumia elimu waliyoipata kujiairi na kuajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa

Aliyasema hayo  jana jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 58 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNICC.

Kwenye mahafali hayo kulikuwa na wahitimu 1,226 wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili (Masters Degree).

Alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua umuhimu wa elimu ya ujasiriamali waliyoipata chuoni hapo kwani itawafundisha namna ya kuwa wabunifu na kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.

“Kwa elimu mliyoipata mnatakiwa kwenda kutengeneza ajira kwa wengine badala ya kuwa tegemezi wa kuhangaika kutafuta kuajiriwa nyinyi nendeni mkajiajiri na kuajiri wengine,” alisema Dk. Hashil

“Nyinyi mmepata elimu bora kwa hiyo nendeni mkaitumie kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayosaidia ustawi wa jamii na chuo kimeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mnapotoka CBE mnakuwa na uwezo wa kujiajiri,” alisema

Alisema utandawazi umesababisha mabadiliko makubwa kwa kasi yanayogusa kila nyanja ya maisha hivyo ni muhimu kutafuta njia ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwenye maisha.

Aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa maono mazuri yaliyisababisha kuanzisha program atamizi ya baishara ambayo inawapa wanafunzi uwezo wa kujifunza usimamizi a biashara kwa vitendo wanapokuwa shule.

Alisema program hiyo na ile ya uanagenzi inawawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakiwa shule hivyo wanapomaliza masomo hawasumbuki kutafuta ajira.

Dk Hashil pia aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuanzisha masomo ya Shahada ya Uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA), mtandaoni kwani inaonyesha ujasiri na uthubutu wa CBE katika kutoa elimu bora na inayokidhi mahitaji ya sasa ya dunia.

“Kuzindua program hizi kunaweka iwango vipya vya ubora   na upatikanaji wa elimu ya juu nawapongea kwa kufungua milango ya fursa kwa wanafunzi na wataalamu ambao wanatafuta kujiendeleza bila kujali umbali,” alisema

Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini na kupongeza mafanikio ya chuo cha CBE na itaendelea kufanyia kazi changamoto ya miundombinu ya vyuo vyote vya elimu ya juu kikiwemo chuo hicho ili kuvuka changamoto hizo.

Alikitaka chuo hicho kuwaendeleza walimu wake na kuwekeza kwenye program za kisasa za kufundisha, mbinu za kujifunza na mitaala ili kuhakikisha elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

“Wekezeni kwenye vifaa vya teknolojia madarasani ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia na chuo kifanye tafiti zinazolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kutoa rasilimali kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika miradi ya utafiti na uvumbuzi,” alisema

Naye Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, alisema wahitimu hao wamehitimu katika masomo mbalimbali yakiwemo ya usimamizi wa biashara, masoko, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na ugavi.

Profesa Lwoga alisema chuo hicho kimejitahidi kwa kiwango kikubwa kuwafundisha wahitimu ili wanapohitimu waweze kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuhangaika kutafuta ajira.

“Tangu mwaka 2022 tulianzisha program atamizi za biashara ambapo wanafunzi wetu wenye mawazo ya biashara na bunifu mbalimbali wanatuletea mawazo yao tunayalea na wanaweza kuanza kufanyabiashara wakiwa chuoni na tunashirikiana na taasisi mbalimbali,” alisema

“Kuna wanafunzi wa CBE wameanza kujiajiri wakiendelea na masomo na kwa sasa wamehitimu tunatarajia waendeleze biashara zao na wakaajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa,” alisema.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, akimtunuku mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakati a mahafali ya 58 ya chuo hicho ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.