November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SERIKALI yaihakikishia kampuni ya Lodhia Group uwekezaji wezeshi

Na Rose Itono, Pwani

SERIKALI imemuhakimishia muwekezaji Lodhia Group kuwa uwekezaji wake wa viwanda nchini hautakwama kwa kuwa ni moja ya kiwanda kinachochangia pato kubwa nnchini

Akizungumza mara baada ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda kipya cha mabati cha Lodhia kinachotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni Kisemvule wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema Lodhia Group ni moja ya Kampuni inayochangia pato kubwa la Taifa

Akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani Pwani Waziri Majaliwa alipata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya kiuchumi sambamba na uwekezaji uliopo katika wilaya hiyo

Alisema kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni ya Lodhia nchini hakuna kiongozi yeyote wa serikali atakayekwamisha jitihada zinazofanywa na muwekezaji huyo ambaye uwekezaji wakeumekuwa ukichangia pato kubwa la serikali kupitia kodi

“Hakuna kiongozi yeyote atakayekwamisha uwekezaji unaofanywa na Lodhia Group badala yake serikali itahakikisha inampa ushirikiano wezeshi utakaomuwezesha kiongozi wa makampuni yanayomilikiwa na muwekezaji huyo kuendelea kuwekeza,”amesema Waziri Majaliwa

Waziri Mkuu akikagua kiwanda cha Lodhia Group ambacho moja ya Kampuni inayochangia pato kubwa la Taifa.

Alimpongeza muwekezaji huyo kwa ushirikiano anaioufanya sambamba na kijitolea kuboresha miunfombinu ya mazingira yanayochangia jamii inayomzunguka kiwandani hapo kuweza kujipatia kipato kupitia biashara mbalimbali

Pia amempongeza kwa kuwa ni moja ya kampuni zinazochangia tatizo la ukosefu wa ajira kwani kupitia kiwanda Cha nondo kiluchopo Kisemvule zaidi ya watanzania 2,000 wamepata ajira na kuweza kuendesha maisha yao.

Amesisitiza kuwa uwezo wa Lodhia Group nchini umetrengeneza fursa kwa wengine kuboresha mazingira kwani baadhi ya wananchi wameweza kufungua biashara mbalimbali zikiwepo Baa, Hoteli na zingine jambao anbali hapo awali halikuwepo kutokana na eneo hilo kuwa pori.

Amewaasa watanzania kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini huku akususitiza kuwataka wafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vinavyomilikiwa na Lodhia Group kujifunza utaalamu wa Teknolojia zinazotunika katika mitambo inayotunika kwenye uzalishaji wa bidhaa Ili nchi iweze kufaidika kwa kuwa na wataalamu wazawa watakaolisaidia taifa baadaye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa makampuni hayo Haroun Lodhia amesema anafurahia kuwekeza nchini na Yuko tayari kushirikiana na watanzania katika kuijenga nchi.

Amesema yeye ni mmoja wa watanzania walioishi kwenye maisha ya umasikini, allikulia Musoma na kula chini kwenye nyumba ya manyasi lakini Leo anamiliki kiwanda Cha kutengeneza mabati hili ni jambo kubwa.

Amesema huu ni mwanzo na anaahidi kufanya makubwa zaidi na ndoto zake ni kuwa muwekezaji mkubwa Afrika Madhariki katika kuzalisha bidhaa zinazotikana na chuma na plastiki.

Amesema kwa sasa Lodhia imekuwa ikilipa kodi ya Sh. bilioni 22 kwa mwaka na kwamba anatarajia mwakani kulipa mara mbili zaidi kutokana na kuendeleza na uwekezaji.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambapo uwekezaji huo umefanyika Abdala Ulega ameongeza kuiiomba serikali kuona namna ya kuwepo na gari la zima moto maenro ya karibu na uwekezaji huo Ili itakapotokea tatizo lolote jamii isidhurike

Amesema kutokana na uwekezaji mkubwa wa Dola za kimarekani milioni 50 uliofanywa na Lodhia ipo haja ya serikali kuona sababu ya kuimarisha usalana kwa kuwa na gari la zima moto ili kuzuia majanga mara tu yatapojitokeza

Hata hivyo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuipanua barabarakuanzia Mbagala hadi Mkuranga na kujifanya iwe njia nne Ili kurahisisha upitaji kwani kwa sasa barabara hiyo imebana sana jambo ambalo serikali imekubali na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuandika barua mara moja TAMISEMI kwa ajili ya kuomba gari la zima moto.

Lodhia Group ni moja ya makampuni makubwa nchini yanayozalisha bidhaa mbalimbali za viwandani zikiwepo nondo mabomba na plastiki za aina mbalimbali