January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yahimiza ushirikishwaji zaidi anuani za makazi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Pwani

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya amehimiza Ofisi za Umma na Ofisi Binafsi kuweka anuani za makazi katika majengo ya Ofisi zao ili kuwa mfano kwa wananchi wengine. Anuani hizo zitasadia kuonesha jina la Ofisi yenyewe Mtaa iliyopo na eneo ambalo posti kodi hiyo ipo.

Naibu katibu Mkuu Mmuya amesema hayo katika ziara yake Mkoani Pwani tarehe 13 /05/2022 alipotembelea na kupokea taarifa ya Mkoa ya utekelezaji wa Anuani za makazi. Kwa sasa ngazi ya Taifa tumefikia 90% ya matarajio yetu lakini tunazidiana Mkoa na Mkoa.

Amepongeza Mkoa wa Pwani kwa kutekeleza vyema zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na kufuata miongozo iliyowekwa katika utekelezaji wa anuani za makazi. “Ziara imelenga kujionea uhalisia ili mwezi huu, tutumie kurekebisha dosari chache tulizogundua kwa kupokea taarifa kwenye mfumo au kwa ziara mbalimbali tunazozifanya au taarifa tunazopatiwa alisema, Naibu Katibu Mkuu Mmuya”

“zoezi la anuani ya makazi ni endelevu, kila mmiliki mwenye eneo ambalo limejengwa au halijajengwa anapaswa kuwa na namba,alisema Naibu Katibu Mmuya”. Hiyo itasaidia kujua mahali eneo lilipo, wananchi wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya umuhimu wa zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na itaongeza dhana ushirikishwaji wa wananchi.

Akihitimisha Kaimu Injinia wa Tanroad Mkoa wa Pwani Meneja Heririsper Mollel amesema utekelezaji wa anuani za makazi umefika katika hatua nzuri ukamilishaji wake kwa sasa wamejikita katika kurekebisha vibao vilivyokosewa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika ziara yake kukagua utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi katika Mkoa wa Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya akiangalia kibao cha anuani za makazi kilichowekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar akipokea taarifa ya utekelezaji wa anuani za makazi ya Mkoa wa Pwani kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Bwn. Ramadhani Mbura, (aliyesimama) kujionea utekelezaji wa zoezi hilo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bwn. Yona Mwakilembe, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya mara baada ya kuwasili kwa ajili kujionea utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi katika Mkoa wa Pwani.