Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako (Mb) amezungumza na vyomba vya habari kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya usalama na afya mahali pa kazi na kusema kwamba lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu mahala pa kazi.
Prof. Ndalichako ameyaeleza hayo leo tarehe 27 Aprili, 2022 wakati wa mkutano na wandishi wa Habari kuhusu kilele cha maadhisho ya usalama na afya mahali pa kazi, Jijini Dodoma. Aidha, amefafanua kuwa takwimu zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani kwa mwaka huu zinaainisha kuwa inakadiriwa zaidi ya watu milioni mbili na laki tisa (2.9 milioni) hupoteza Maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
“Kupitia takwimu hizo tunaweza kupata picha na uzito wa changamoto ya madhara yanayo sababishwa na mazingira ya kazi yasiyo rafiki kwa wafanyakazi na ndio maana mwaka huu Shirika la Kazi Duniani limeamua kaulimbiu kuwa ni : kwa pamoja tushirikiane kujenga utamaduni bora wa usalama na afya mahali pa kazi “ alisema Prof. Ndalichako.
Aidha alibainisha kuwa kwa hapa nchini tulianza kuadhimisha siku hii tangu mwaka 2004 ambapo maadhimisho hayo yamekuwa yakiratibiwa na Serikali kupitia Taasisi yake ya OSHA kwa kushirikiana na Wadau wa Utatu ambapo ni Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi- TUCTA na Chama cha Waajiri Tanzania- ATE pamoja na Shirika la Kazi Duniani-ILO. Vilevile Alisema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika Jijini Dodoma.
Aidha alisema kama Nchi inashiriki katika kampeni ya kidunia kwa kufanya mambo mbalimbali yanayolenga kukuza uelewa wa masuala ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi na kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni bora wa Usalama na Afya katika shughuli za kiuchumi za kila siku.
More Stories
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani
Rais Samia apeleka neema Tabora
Samia apeleka neema Tabora, aidhinisha Bil. 19/- za umeme