Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. samia Suluhu Hassan amesema Serikali inazidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ambapo imejenga kituo cha kupokea na kupoza umeme wilayani Kongwa mkoani Dodoma ambacho kitaboresha pia hali ya umeme wilayani Gairo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Agosti 02, 2024 wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi.
Aidha Rais Samia amesema kuwa, njia ya umeme kutoka kituo cha kupoza umeme cha Kongwa kwenda wilayani Gairo imeshakamilika.
Rais Samia amesema kila kwenye maendeleo hakukosekani changamoto hivyo amewaahidi wakazi wa Gairo kwamba changamoto zao zote zinakwenda kufanyiwa kazi.
Kwa upande wa Maji katika Jimbo hilo, Rais samia amesema serikali imepeleka shilingi Bilioni 34 na mikataba mbalimbali imesainiwa ambapo tayari kazi imeanza kuhakikisha Gairo inapata maji ya kutosha
Mbali na Hayo, Rais Samia amewataka wakazi wa Gairo kuendelea kudumisha
amani na utulivu ili serikali iendelee kufikiroa maendeleo zaidi huku akiwataka wakazi hai kuzalisha zaidi mazao ya biashara
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa