November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaboresha viwanja vya Ndege 40 pamoja na miundombinu katika hifadhi

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

SERIKALI imeboresha zaidi viwanja vya Ndege 40 pamoja na miundombinu katika hifadhi za ukanda wa kaskazini na barabara zinazofikika kwa urahisi ukilinganisha na ukanda wa Kusini. Imeelezwa kuwa hifadhi ya Taifa Serengeti imekuwa na viwanja vya ndege visivyopungua sita.

“Kikubwa tunachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha tunaboresha miundombinu katika hifadhi zote za kusini na mradi huo utakamilika hadi mwaka 2025 na kazi nyingine ni kuweka mikakati ya namna ya kuvutia watalii ili mgeni anapofika katika hifadhi hizo apate huduma zote muhimu ikiwemo chakula na malazi,” amesema Prof. Sedoyeka.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo ameomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha mazingira kwa ajili ya kuvutia watalii kwa kujenga sehemu za kutoa huduma za malazi na chakula.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Mkuu wa Kanda ya Kusini, Steria Ndaga amesema wanaendelea na jitihada za kuvitangaza vivutio vyote vinavyopatikana katika Hifadhi za Taifa zilizoko kusini.

Aidha amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa vivutio hivyo ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua mkopo kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya ndege katika kila Hifadhi ya Taifa ili kusaidia watalii kutua muda wowote na kila maeneo muhimu ambayo yatawekwa.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imekopa zaidi ya sh. bilioni 350 ili kuwekeza kwenye hifadhi zote zinazopatikana kusini naamini hatua hiyo itasaidia kuongeza na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi, tumezoea kuona idadi kubwa ya watalii ukanda wa kaskazini ni kutokana na uboreshaji wa miundombinu.

Ametaja miundo mbinu kuwa ni pamoja na viwanja vya ndege barabara na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Mkuu wa Kanda ya Kusini, Steria Ndaga amesema wanaendelea na jitihada za kuvitangaza vivutio vyote vinavyopatikana katika Hifadhi za Taifa zilizoko kusini.

Ndaga amesema lengo la kutangaza vivutio hivyo ni kufungua fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zitawavutia watalii kutembelea hifadhi hizo na kutafuta taarifa sahihi za uhifadhi katika maeneo hayo.

“Tunaamini kuwa vivutio hivi itakuwa fursa tosha kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.” amesema.