December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali ya Mkoa wa Dar yawaasa wahitimu amana

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

VIJANA wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita kwa kuendeleza taaluma walizozipata vyuoni mwao.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Septemba 6, 2024 katika mahafali ya 27  mgeni rasmi katika hafla hiyo  alikuwa afisa maendeleo ya vijana mkoa wa Dar es salaam Mh.Masalida Zefania alianza kwa kuwapongeza wahimu hao na kusema kwamba wahakikishe wanaziendeleza taaluma zao.

“Nawaasa wahitimu wa chuo cha amana vijana center, najua Leo mkoa katika furaha kwa kuhitimu masomo kwa ngazi ya cheti hivyo fanyeni jitihada muutumie ujuzi huo kwa kutafuta  fursa za ajira ama kujiajiri sehemu mbalimbali,” amesema Zefania

Aidha Zefania ameeleza kwamba mbali na juhudi za utoaji wa mafunzo  kwa  vijana amana vijana center inatoa kozi kwa watu wenye mahitaji maalumu  ambapo ameahidi kukisaidia kupunguza baadhi ya changamoto.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo hicho Philipo Ndokeji amewataka wahitimu hao kutumia taaluma zao vizuri katika kuziendea fursa mbalimbali za ajira.

Mkuu huyo amewasihi vijana hao kuzingatia nidhamu kwani ni sehemu muhimu  katika kutekeleza majukumu yao, isitoshe ndio kitu pekee kinachofungua milango ya ajira  mahala popote duniani.

Nae mhitumu wa kozi ya hoteli aliyejulikana kwa jina la. Issaya ameahidi kutumia vema ujuzi alioupata chuoni hapo na kuwa balozi wa kukitangaza chuo hicho sehemu mbalimbali.