December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali ya ccm dar yaahidi vifaa saidizi

Baadhi ya wahimu wa chuo cha Ushirika vijana centre Ilala mkoani Dar es salaam wa kozi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali ya 4 ambapo jumla ya 120 walihimu mafunzo hayo,kati yao wavulana walikuwa 48 na wasichana 72

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

SERIKALI ya chama cha mapinduzi(CCM) imeahidi kutoa msaada wa vifaa wezeshi kama Computer ili kukiwezesha chuo cha Ushirika kifikia malengo yake.

Hayo yameelezwa na mgeni rasmi katika mahafali ya 4 ya chuo cha Ushirika mkoani Dar es salaam, ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama Ali Mangungu amesema kutokana changamoto alizozisikia kupitia risala yao, binafsi yake atajitolea mashine ya computer.

“kutokana na changamoto mbalimbali zilizoelezwa hapa serikali ya CCM ipo pamoja na chuo hiki hivyo kwa Ushirikiano huo, mimi nitajitolea baadhi ya vifaa vya kujifunzia ikiwemo mashne Computer, “amesema Mangungu

Aidha Mangungu amewataka vijana wao kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo nchini ili kuitendea haki elimu waliyokuwa yameipata chuoni hapo.

Nae mkurugenzi wa chuo hicho Magoye Machela ameeleza chuo chake ni cha kizalendo kwa vijana wa rika zote ikiwemo wenye mahitaji maalumu ambapo kimewasaidia wengi kufika malengo yao bila malipo .

Mkurugenzi huyo amesama kozi zitolewazo na chuo chake ni pamoja na hoteli managementi, udereva, Air ticketing, saluni, computer, cherehani na kiingereza hivyo jumla wahitimu 120 walimaliza kozi hizo ikiwemo wavulana 48 na wasichana 72 .

Kwa upande wa mhitimu wa kozi ya komputer (graphics) Athuman Hamisi amesema ujuzi alioupata chuoni hapo atakwenda kuufanyia kazi ipasavyo mahala atakapo kwenda.

Mhitimu wa kozi ya Saluni Faty- hiya Abdurazak ameahidi kufungua saluni kubwa ambayo itakuwa ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo urembo na make ups.