Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Serikali,wadau na jamii wametakiwa kuweka nguvu katika hupatikanaji wa vifaa na sehemu ya kujihifadhia watoto wa kike wakati wa hedhi,ili waweze kuwa na hedhi salama itakayochangia kuhudhuria masomo kwa ukamilifu.
Huku wanaume wakitakiwa kuvunja ukimya na kuachana na mila na desturi za zamani badala yake wawe mstari wa mbele kuhakikisha watoto wa kike na wanawake wanapata taulo za kike, sehemu za kujihifadhia na kutunza taulo hizo baada ya kutumia.
Akizungumza na timesmajira online, ofisini kwake mkoani Mwanza Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Haki Zetu Tanzania Evodius Gervas,ameeleza kuwa changamoto katika masuala ya hedhi imekuwa ni kubwa kwa sababu imekuwa haishughulikiwi vizuri.
Gervas , ameeleza kwa pamoja waelekeze nguvu katika suala hilo ili watoto wa kike waweze kuwa kwenye mazingira ambayo ni salama kwao,waweze kupata sehemu nzuri ya kujihifadhi na kutunza taulo za kike ambazo zimeisha tumika.
“Kwa sababu utasikia sana kampeni za masuala ya hedhi pale inapofika Mei 28 ya kila mwaka ndio unasikia watu wanaanza kuongea lakini hedhi ipo kila siku na haisubili siku hiyo pekee, mimi naona bado haijawekwa nguvu na tunaposema hedhi salama tunamaanisha mtoto wa kike au mwanamke anapata mahitaji yake ambayo ni muhimu wakati wa hedhi,”ameeleza Gervas.
Ameeleza kuwa,ukiangalia bei ya kununua vifaa vya kujihifadhia zipo juu ambazo siyo rafiki kwa baadhi ya watu kwa mfano ukiangalia vijijini ni familia chache ambazo zinaweza kumudu kuwanunulia watoto wao taulo za kike.
Amesema,utokana na hali hiyo wanaamua kutumia vitu ambavyo siyo salama labda wanatumia vitambaa lakini ukiangalia vile vitambaa siyo salama maana wataalamu wanashauri mtu atumue kitambaa ambacho ni cha pamba kitakachoweza kufyonza uchafu na kiwe ni kisafi kianikwe sehemu nzuri na kupigwa pasi.
“Ukiangalia mazingira ya kijijini pasi ya kutumia kwa ajili ya kupasi vitambaa wanaitoa wapi,hicho kitambaa cha pamba wanakitoa wapi kwaio anachofanya anatumia kitu chochote ili mradi hajistiri kwaio inasababisha madhara mengine,ninafikiri kwamba kama serikali inaweza kutoa mipira ya kiume bure naamini inaweza kutoa hata taulo za kike bure kwa watoto hasa wale ambao wako shuleni na basi kama siyo bure iweke ruzuku ili ziweze kupungua gharama,”ameeleza Gervas.
Pia amesema,hedhi ni maisha ya watu,ni afya ya mtu siyo kitu cha kuweka kodi yeye anaamini kwamba na wakati wote anawaambia rafiki zake kuwa zawadi ambayo utamnunulia mke wako akaifurahia ni taulo ya kike au vifaa kwa ajili ya kujiihifadhi wakati wa hedhi.
“Sisi wanaume tujenge tabia ya kwenda kununua taulo za kike na kuwapelekea wake zetu,watoto wetu wa kike na wengineo hii itasaidia sana na tutaona kwamba tunawajibu wa kuwalinda na kuhakikisha kwamba wanapata mazingira salama,”.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best