
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Ndugu Afraha Hassan amesema Serikali inakusudia kuweka uzio wa umeme wenye thamani ya shilingi Billioni 7 katika kata tano (5) zinazozunguka maeneo ya hifadhi ya Lwafi ambao utasadia kudhibiti Wanyama waharifu aina ya Tembo kuharibu mazao ya wananchi.
Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo hayo na kusema uwepo wa uzio huo utakuwa suluhisho la kudumu katika kuwadhibti Wanyama hao na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subra wakati swala hilo likiendelea kufanyiwa kazi.
‘’suluhisho la kudumu litapatikana baada ya kuwekwa uzio wa umeme ni waya mfupi unaopitishwa kwenye vigingi, unakuwa mmoja au miwili, tembo akifika unampiga shoti,hivyo anakuwa anashindwa kuvuka Gharama yake ni kubwa ni takribani Billion saba hivi’’alisema Hassan.
Kwa upande wake Afisa Wanyama Poli Wilayani humo Anod Shadrack Ngagashi,alisema licha ya hilo Serikali inakusudia kuongeza doria katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kufanya malipo ya fidia kwa wananchi wote waliokubwa na kadhia ya kuliwa na mamba ambapo kwa mwaka 2026 watu 41 wamelipwa.
Hata hivyo mikutano hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Dkt Mwigulu Nchemba alioyo yatoa baada ya kufanya ziara wilayani humo juu ya viongozi wa Serikali kujikita katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi

More Stories
Diwani Bhojani atoa nguo kwa watoto Ilala
Maeneo 65 yapendekezwa kwa wachimbaji wadogo hasa vijana
Kutoka ndoto hadi furaha,umeme kumfikia Sesilia