Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma amesema kuwa Serikali itawapatia kila mmoja zawadi ya shilingi 500,000 washiriki 6 walioingia Fainali ya Bongo Star Search msimu wa 14 ikiwa ni kuunga mkono jitihada mbalimbali za sekta binafsi katika kuibua vipaji vya vijana kwenye tasnia ya Sanaa.
Mwinjuma ameyasema hayo Baada ya kuvutiwa na vipaji vilivyoonyeshwa na vijana hao wakati wa Fainali za Shindano la kutafuta vipaji la Bongo Star Search ambapo amewapongeza washiriki wote kwa namna walivyoonyesha uwezo wao hivyo ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye shindano hilo na Sanaa Kwa ujumla.
Pia Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma alipokea Tuzo iliyotolewa na waandaaji wa shindano la kuibua na kusaka vipaji la Bongo Star Search kwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kutambua jitihada mbalimbali anazozifanya katika kukuza na kuendeleza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.
Kwa upande wake Chief Judge Msrita Paulsen alitoa shukrani dhati kwa watu wote waliochangia kuifanikisha bongo star search Season 14 kuanzia ilipoanza hadi ilipofika kikomo.
Fainali hizo zilizofanyika usiku wa Januari 27 2024 katika ukumbi wa Warehouse Dar es salaam ambazo zilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Gerson Msigwa pamoja na Mtendaji Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Dkt. Kedmon Mapana.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa