Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
NAIBU Waziri wa Ofisi Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema Serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi zinazowachukua Vijana wanaofanya mafunzo ya vitendo ili kuwajengea uwezo, kupunguza tatizo la ajira na kufungua fursa za kiuchumi nchini
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri Patrobas Katambi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika baadhi taasisi za serikali na binafsi kujionea Kitengo cha Huduma za Ajira (TAESA) mafunzo ya Elimu ya ngazi mbalimbali wa kupata ujuzi na uzoefu ule ambao waajiri ili kuweza kushindana na soko la ajira.
“Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba 2022, Serikali imeweza kutoa ajira nje ya nchini kwa vijana 92 katika nchi za Poland, Imani na Saudi Arabia”, Pia Serikali inaendelea na mazungumzo na nchi ya Saudi Arabia ambapo vijana 450 wanatarajia kupata ajira, Omani ikitarajia kuajiri vijana 382 wanaotarajia kupata ajira katika nchi hiyo.
Kwa upande wa nchi ya Qatar, tayari vijana wa kitanzania wameenda kufanya kazi hasa kipindi hiki cha kombe la dunia.”Hii Ni jitihada ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa tunatatua changamoto ya ajira nchini ikiwemo kubadilisha mitaala ya Elimu ili iweze kuendana na mahitaji ya Sasa”.
Sambamba na Hilo kumekuwa na kazi kubwa inayofanyika kwa kujaribu kufungua mipaka ili wawekezaji waje nchini na kukuza Sekta binafsi ili iweze kupata ajira, hivyo miradi mikubwa ya kiserikali imekuwa ni eneo kikubwa la kutoa ajira kwa vijana, ambapo bwawa la Mwalimu Nyerere limetoa ajira kwa vijana 7500, bomba la mafuta litatoa ajira zaidi ya 500,000
kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAESA Joseph Nganga amesema Naibu Waziri alikuwa anatembelea katika baadhi ya tasisi zinazoshirikiana na Taesa kuwa Kama darasa la Vijana wanaofanya mafunzo kwa uzoefu wa kazi (Internship).
Programu hiyo imekuwa ni muhimu kwa vijana wanaihitimu vyuo na kupewa mafunzo ya Elimu ya ngazi mbalimbali wa kupata ujuzi na uzoefu ule ambao waajiri wanautaka.”Nawashukuru waajiri wote zaidi ya 200 kwa muda Mwaka mmoja wa kuwapa mafunzo na wanapotoka huko wanakuwa katika ujuzi unaohitajika”
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa