Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amesema Serikali inaendelea kufanya jitihada za kukuza kilimo cha alizeti ili nchi iweze kuzalisha kwa wingi mafuta ya kupikia na kuondokana na uhaba wa bidhaa hiyo.
Aidha amesema,Jeshi la Kujenga Taifa ni miongoni mwa taasisi za Serikali ambapo limekuwa likizalisha mazao ya mafuta likiwemo zao la alizeti.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo jijini Mbeya wakati akihitimisha ziara yake kwenye maonyesho ya wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
“Serikali inaendelea kufanya jitihada za kukuza kilimo cha alizeti,hata upade wa JKT inaendelea kuweka jitihada kubwa katika uzalishaji wa zao hilo ambalo faida zake ni nyingi ikiwemo kuokoa fedha za kigeni tunazotumia kuagiza mafuta nje ya nchi,
“Kwa hiyo mkakati wetu ndani ya serikali kupitia jeshi ;a kujenga Taifa ni kuongeza mawanda ya uzalishaji kupitia JKT maana hata matajitri wanatafuta sana mafuta haya ,sasa kwa vile mwenyezi Mungu ametujalia ardhi nzuri na mikoa mingi zao hili linastawi vizuri basi JKT litakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wizara ya kilimo kuongeza uzalishaji wa zao hilo na mazao mengine .”alisema Bashungwa
Aidha alisema JKT pia limesaini makubaliano na Wizara ya Kilimo ambayo yanaenda kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji na kutoa mchango katika mageuzi ya kilimo nchini.
“Lakini pia kesho (Agosti 3,2023)Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi zitashuhudia JKT likitiliana saini Mkataba na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuhakikisha vijana wa JKT wanajengewa uwezo utakaowawezesha kujitegemea kupitia sekta za mifugo na uvuvi pindi wanapomaliza mkataba wao wa mafunzo ya JKT.
Alisema,hatua hiyo hatua hiyo itaenda kusaidia vijana hao kujiajiri lakini pia kuchangia katika pato la Taifa.
“Takwimu zinaonyesha asilimia 45 tu ya vijana wa kujitolea ndiyo wanapata ajira katika vyombo mbalimbali vya majeshi na asilimai 55 inayobaki ya vijana wanarudi uraiani baada ya kumaliza mktaba wao JKT,sasa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona hiyo asilimia 55 ya vijana wanaohitimu mkataba wa kujitolea JKT inapata ajira.”alisema Waziri Bashungwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT Kanali Peter Lushika amesema, JKT lina mchango mkubwa hasa katika uzalishaji wa mazao mbalimbali hapa nchini ambapo wameweza kuimarisha zaidi usalama wa chakula katika maeneno ya mbalimbali huku akitaja eneo mojawapo kuwa ni eneo la uzalishaji wa mbegu katika mashamba ya JKT.
Aidha amesema,kazi wanayoifanya katika banda lao kwenye maonyesho hayo ni pamoja na kufundisha vijana na kutoa elimu kwa wananchi kwa ujumla kuhusu teknolojia katika kilimo na matumizi sahihi ya pembejeo ,matumizi ya mbolea na mbegu zinazolishwa ili kufahamu na kulima kilimo chenye tija.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato