Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM
SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam imesema itatatua changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo cha Amana vijana center kwa kuanzia imeahidi kutoa viti vipatavyo 100 kwa lengo la kuwasaidia vijana wanaopata Elimu mahala hapo.
Hayo yamesemwa katika hafla ya 25 ya chuo hicho ambapo vijana 252 wamehitimu mafunzo katika kozi mbalimbali ikiwemo hoteli management, saluni,mapambo na kiingereza.
Akizungumza katika mahali hayo katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Dar es salaam Ali Bananga amesema tunakila sababu za kukisaidia chuo hiki kwa sababu kinajitolea kusaidia mamia ya vijana wetu kupata ujuzi.
“Kutokana na mazingira yalivyo tunakila sababu ya kukisapoti chuo cha Amana kwa kuwa kinajitoa kuwasaidia vijana wetu kupata ujuzi wezeshi Ili kukabiliana na ajira ama kujiajili,” amesema Bananga
Aidha Bananga amewataka wazazi wa wahitimu kuwaendeleza vijana wao Ili waweze kuwafaa siku za usoni majumbani au kwenye sekta mbalimbali za kazi.
Kwa upande wa mkurugenzi wa chuo hicho Philipo Ndokeji amewataka wahitimu hao kuzingatia nidhamu na maarifa amesema ndio msingi wa mafanikio katika maisha .
Ameeleza kozi zitolewazo na chuo hicho ni pamoja na kiingereza, kompyuta, hotel management, saluni na mapambo hivyo kutokana na fursa hiyo amewata vijana ambao wapo vijiweni kujiunga na masomo hayo
Nae mhitimu wa kozi ya hoteli aliyejulikana kwa jina la Saidi Yahya amesema ujuzi alioupata chuo hapo atautumia vema Ili kuweza kukabiliana na changamoto za maisha ikiwemo kuwasaidia wazazi wake.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake