Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Mbozi.
SERIKALI imesema inajenga vyuo vya VETA katika kila Halmashauri ili kuwapa vijana ujuzi utakaowawezesha kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana kwenye maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananachi Wilaya ya Mbozi alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayounganisha maeneo ya Ruanda, Nyimbili, Hasamba, Izyila na Itumba yenye urefu wa Kilometa 79.67 ambayo pia itaunganisha maeneo ya Mahenje, Hasamba, Vwawa kwa urefu wa Kilimita 31.9 inayojengwa kwa kiwango Cha lami.
Amesema wanaanza na Halmashauri 28, kwa mwaka huu wa fedha zitajengwa Halmashauri 48 lengo ikiwa Halmashauri zote 184 zijengwe VETA kwaajili ya vijana hao.
“Tunajenga VETA mikoa yote na sasa tunajenga VETA Kila Halmashauri, malengo yetu ni vijana wetu hawa waliopo majumbani wale waliomaliza darasa la Saba, kidato cha nne hata waliopo madarasani wanapomaliza, huwa tunatoa tangazo la kujifunza Ufundi mbalimbali kwenye VETA, tunataka vijana wasibaki mtaani bila kuwa na ujuzi”
“Tunataka tuimarishe vyuo ambavyo vijana wenye mahitaji maalumu watakwenda kupata Taaluma na wao wapate ujuzi, elimu ili waweze kushiriki kwenye shughuli za kutuletea maendeleo nchini”amesema Majaliwa
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea kupata vibali kutoka ofisi ya Rais kuongeza idadi ya walimu katika shule ya msingi Ruanda ili waende kuongeza nguvu mashuleni.
“Walimu katika shule ya msingi Ruanda wapo inawezekana hawatoshi, hivyo walimu endeleeni kufanya kazi yenu vizuri, serikali inaendelea na kupata vibali kutoka ofisi ya Rais kuongeza idadi ya walimu, hivi karibuni tumeshapata kibali Cha watumishi walimu 4000 kwaajili ya shule za msingi, na 2000 kwaajili ya shule za sekondari ili waje kuongeza nguvu”
Kuhusu walimu kulipwa madeni yao, Waziri Mkuu Majiwa amesema tayari wameshaanza kulipa yale madeni ambayo walikua wanayadai, ambapo kwa Wilaya ya Mbozi wamelipa kwa zaidi ya asilimia 80.
“Kama kuna walimu hapa msisite kupeleka madai yale kwa Afisa elimu ili waje wajiridhishe na wataalamu wetu wa hesabu wa Halmashauri ili na nyinyi mpate kulipwa,”amesisitiza
Majaliwa amewahakikishia walimu wote ambao bado hawajapandishwa madaraja kuwa zoezi hilo linaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo na kulipwa malimbikizo yao.
“Upandashaji madaraja kwa walimu unaendelea, wale mliochelewa kupanda madaraja TSC iwemo, inakusanya takwimu zenu na kuwapandisha madaraja, hatakama ulilukwa, wanachofanya sasa ni wanawavusha kutoka hapo mlipo kwenda ambapo wenzenu walipo kwa mujibu wa Taaluma yenu na unalipwa malimbikizo yenu yote”
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa