Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema Serikali inajenga zaidi ya miradi 1,000 katika maeneo mbalimbali kote nchini ili kuwasogezea huduma ya majisafi na salama wananchi wake.
Mhandisi Sanga amesema hayo Oktoba 13, 2022 wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Mbalache-Lupombwe.
“Kila kona ya nchi hii kuna mradi unajengwa na niwahakikishie miradi mingi inayojengwa kipindi hiki ni miradi yenye ubora mzuri na hata kwenye Mbio za Mwenge mwaka huu miradi iliyokaguliwa ilipongezwa na viongozi wa mbio za mwenge,” amesema Mhandisi Sanga.
Mhandisi Sanga amewapongeza wataalam Wizara ya Maji kwa kuhakikisha ubora wa miradi lakini pia aliwapongeza Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi Wilayani Makete kwa jitihada zao, ufuatiliaji na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji wilayani humo.
More Stories
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana