November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kujenga Gati jipya kuhudumia makaa ya mawe na Sement-Mtwara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inaendelea kununua mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuhudumia Bandari ya Mtwara pia kujenga Gati jipya eneo la kisiwa Mgao kwa ajili ya kuhudumia bidhaa za Makaa ya Mawe, Cement na Mbolea.

Mbarawa amaeyasema hayo Baada ya kukagua utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara Pamoja kutembelea eneo la Kisiwa Mgao ambapo panatarajiwa kujengwa geti jipya.

“Serikali ipo katika hatua ya Mwisho ya kumtafuta ya kumpata mkandarasi wa kujenga gati jipya katika eneo la kisiwa Mgao ili gati hilo liweze kuhudumia bidhaa kama vile Makaa ya Mawe, Sement na Mbolea” Alisema Prof. Mbarawa.

Pia Prof Mbarawa amesema kuwa uboreshaji wa Bandari ya Mtwara umeongeza fursa kwa vijana kupata ajira pia mzunguko wa fedha umeongeza .

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Rajab Kundya amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa uafanisi katika Bandari ya Mtwara pia fursa kwa vijana wa Mtwara Imeongezeka na kufanya Mtwara vijana wengi kujishughulisha na kazi mbalimbali.

“Pia uboreshaje wa Bandari ya Mtwara umevutia nchi ya Msumbiji na Visiwa vya Comoro kutumia bandari hiyo kwa ajili ya kusafirsha bidhaa mbalimbali kama vile Sement mazao ya chakula”Alisema Rajab Kundya

Meneja wa Bandari ya Mtwara Ferdinand Nyathi amsema kuwa pamoja na Bandari hiyo kusafarisha Korosho lakini serikali imenunua mitambo ya shilingi Bilioni 36 kwa ajili ya kuhudumia bidhaa Mchanganyiko na tayari mtambo huyo umeshawasili katika Bandari ya Mtwara na Mtambo mwaingine unatarajia kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.