Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Serikali imesema inakwenda kwenye hatua ya kufanya ukaguzi kama fedha zilizotengwa na serikali kwajili ya walemavu zinawafikia ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya kujua fedha hizo zinawafikia kwa kiwango gani.
Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa chuo cha ufundi stadi na marekebisho cha Masiwani Jijini Tanga.
Naibu waziri Katambi Halmashauri zote nchini zinaendelea kuelekezwa kwamba katika kutenga fedha nchini hiyo asilimia 2 iendelee kutolewa ili kuhakikisha kwamba fedha zote zinazokusanywa zinatolewa asilimia 2 kwajili ya watu wenye ulemavu.
“Halmashauri zote zimeendelea kuelekezwa kwamba katila kutenga fedha nchini hiyo asilimia 2 kwajili ya walemavu iendelee kutolewa tunataka nao wajione ni sehemu ya jamii yetu, “alisistiza Naibu waziri huyo.
Aidha Naibu waziri Katambi amesema serikali inatumia zaidi ya bilioni 3 kwajili ya kujenga vyuo vya ufundi stadi vya walemavu nchini Tanzania.
Alisema hatua hiyo inaiwezesha jamii hiyo kujiajiri na kuwa na sifa ya kuajirika na hatimaye kuondokana na utegemezi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la NSSF Mashaji Mshombe amesema jukumu la msingi la kutoa na kusaidia jamii katika masuala muhimu kwa maendeleo ya Taifa mojawapo ni elimu, afya hivyo kwa kutambua hilo moja ya vipaumbele vyao mubimu katika masula ya kijamii ni usaidizi huku wakizingatia msimamo wa serikali ya awamu ya 6.
“Tunaendelea kuweka msisitizo wa kuongeza nguvu katika vyuo vya ufundi kadri ambavyo mheshimiwa Rais anavyosisitiza na ndio maana hatukusita pale tulipoona kuna nafasi ya kusaidia hapa Masiwani basi tukaweka nguvu na ndio maana leo tuko hapa, “alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake katibu tawala Mkoa wa Tanga Pili Mnyema amesema Mkoa wa Tanga umetumia kiasi cha shilingi milioni 121 kwajili ya ya kuwawezesha watu wenye ulemavu.
Mkuu wa chuo cha walemavu Masiwani Joyria Msuya na Mbunge wa viti maalumu Kigoma Zainab Katamba wameitaka jamii kuwapenda watu wenye ulemavu.
Joyria Msuya aliishukuru ofisi ya waziri mkuu kwa kuwajengea chuo hicho huku akisema vyuo vya watu wenye ulemavu nchini sio vyuo vya watu wagonjwa bali ni vyuo vya watu wote pamoja na wale waliopata ajali zinazosababisha ulemavu na tayari wameshajikubali, wanajiamini na wametambua kuwa ulemavu siyo kikwazo kwao.
Maeneo ambayo yamejengwa vyuo vya walemavu Nchini ni Daresalam, Tabora, Singida, Mtwara, Mwanza na Tanga.
Malengo makuu ya kuanzishwa chuo cha Masiwani na vyuo vingine ilikuwa ni kuwapa elimu ya ugundi na biashara vijana wenye ulemavu itakayowawezesha kuanzisha miradi yao midogo midogo ya uzalishaji mali ili waweze kujitegemea pindi eakimaliza mafunzo yao na kurudi makwao au wawezevkuajiriwa.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM