Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
SERIKALI inaandaa utaratibu wa kuhakikisha kuwa wazee wasiojiweza kugharamia matibabu wanafuika na mpango wa Bima ya afya kwa wote ambao utaanza mara baada ya sheria kutungwa bungeni .
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa kanda mbeya (MZRH), Dkt. Godlove Mbwanji wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu mswada wa bima ya afya kwa wote iliyofanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo .
Dkt Mbwanji amesema kuwa serikali inaendelea kuweka utaratibu wa matibabu kwa wazee wasiojiweza ili waweze kupata matibabu .
Mkurugenzi huyo amesema kuwa zipo familia ambazo hazina uwezo serikali itakuwa na utaratibu wa kuwatambua wazee wote na kuhakikisha wanapatiwa matibu bila wasiwasi wowote .
“Lakini kumeendelea kuwepo kwa maboresho mbali mbali ambayo yamepelekea umri wa kuishi binadamu kuongozeka mimi nawafahamu wazee waliostaafu mwaka 1993 katika taratibu za bima unaweza useme bima inaingiliwa lakini bado wanapatiwa matibabu ”alisema.
Ameongeza“,lakini hatupo hapa kufurahi watu kupoteza maisha na kazi yetu ni kuhakikisha kila mtanzania apate huduma kwa hiyo wazee wao kuna sera inasema bima bure tumeweka kwa wazee wasiojiweza pia tumekuwa tukipata changamoto nyingi “amesema mkurugenzi huyo .
Hata hivyo Dkt.Mbwanji amesema inawezekana baadhi ya wazee wakapata matibabu kupitia kwa watoto wao lakini kwa wale wasio na uwezo serikali itakuwa na utaratibu wa kuwatambua katika ili waweze kupatiwa matibabu .
Mwandishi wa habari Mbeya yetu online Tv Ezekiel Kamanga amesema kuwa unapoelekea mchakato wa bima ya afya kwa wote wazee hawajawekwa kwa sababu ya Sera ya wazee inawataka kupata matibabu bure kuanzia kwenye zahanati , vituo vya afya ,hospitali za wilaya mpaka rufaa.
“ Bima ya afya kwa wote haijasema popote ni vema serikali kuanisha watapataje huduma kupitia mpango huo kwa sababu tayari wengi wao walishalitumikia taifa ,wakulima , wafanyakazi kwenye serikali na kuwa unapofika miaka 60 bima inakomaa ukishastaafu.
Aidha ametoa wito kwa waandishi wa habari kuwa mabarozi wazuri wa kuelezea bima ya afya kwa wote kwa wananchi ili waweze kuifahamu .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa mbeya ,Nebart Msokwa amesema sema kuwa kundi la waandishi wa habari ni muhimu katika kuelimisha jamii .
“Zipo taasisi nyingi ambazo zinafanya kazi na sisi lakini nyie mmetukumbuka kutupa elimu hii muhimu ya kuelimisha jamii kuhusu bima ya afya kwa wote ,lakini kukiwa na mambo muhimu kama haya huwa mnatukumbuka lakini wakati mwingine tuitwe kupeana elimu mbali mbali “amesema Msokwa.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia