November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sensa ya 2022 kupata watu milioni 61.3

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa Sensa ya sita ya mwaka huu 2022 inakadiriwa kupata watu milioni 61.3

Hayo ameyasema Leo (Juni 14, 2022) Mtaalam wa Idadi ya watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hellen Siriwa huko Mkoani Iringa, wakati wa mafunzo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) yakiwa na lengo la kuwajengea uwelewa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Hellen amesema Sensa ya kwanza ya mwaka 1967 ilipata ya watu milioni 12.3, sensa ya pili ya mwaka 1978 ilipata watu milioni 17.5, sensa ya tatu ya mwaka 1988 ilipata nidadi ya watu milioni 23.1, sensa ya nne ya mwaka 2002 ilipata watu milioni 34.4 na sensa ya tano ya mwaka 2012 ilipata idadi ya watu milioni 44.9

Aidha mtaalam huyo wa idadi ya watu na makazi amesema sensa ya mwaka huu itatoa majawabu katika mambo mbalimbali ya msingi;

“Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa nyingine zilizotangulia itatoa majawabu katika mambo ya msingi yanayohusu watu kiafya, kielimu, kijamii, kimazingira na kiuchumi”

Aidha amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya kufanya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kuunganisha mazoezi mengine mawili makubwa ya kitaifa ambapo tangu tulipopata uhuru hatukuwahi kuwa na sensa ya majengo na ndiyo inafanyika ndani ya serikali ya awamu ya sita huku ikifanyika kwa weledi, dhamira ya kweli na utaalamu wa kutosha.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mary Senape amesema Ni Kinyume cha Sheria za Takwimu Kutoa taarifa/takwimu za uongo, Kumshawishi mtu asishiriki zoezi la Takwimu, Kujifanya Afisa wa Takwimu na Kutumia Takwimu za Sensa kwa taarifa zako binafsi

Naye Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Said Amir amesema mafunzo hayo ni sehemu ya Programu ya uhamasishaji ushiriki wa vyombo vya habari katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022

“Tumeanza na vyombo vya habari vya mtandaoni, tutakutana pia na makundi mengine ya waandishi wa habari wakiwemo Wahariri, Jukwaa la wahariri na Radio za Mikoani”,amesema Ameir.

“Katika mafunzo haya ya siku mbili waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii watajengewa uwezo/uelewa kuhusu Sensa na Sheria ya Takwimu,umuhimu wa sense ya watu na makazi na maandalizi yake,madodoso ya sense na maudhui yake, maeneo ya kuhesabia watu ya sense ya watu na makazi ya mwaka 2022,Matumizi ya Teknolojia katika senda ya watu na makazi kutoka kwenye makaratasi hadi kwenye Kishikwambi”,amesema Amir.

Mbali na hayo, Amir amesema wao Kama NBS wamepewa jukumu la mushughulikia takwimu za uchumi, kijamii na maizingira;

“NBS tumepewa jukumu la kushughulikia takwimu za Uchumi, Kijamii na Mazingira

Katika Uchumi tunashughulikia pato la Taifa, Mfumuko wa bei, Madini, Kilimo n.k

Katika Jamii tunashughulikia Maji, Umeme, Afya

Na katika Mazingira tunashughulikia Hali ya hewa”