Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Diwani wa Kata ya Gongolamboto Lucas Lutainurwa amewapongeza Walimu wa shule ya Sekondari Juhudi Wilayani Ilala kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024.
Pongezi hizo Diwani Lucas akizitoa shuleni hapo kwa kuwapa zawadi sehemu ya motisha ili waendelee kufanya vizuri na kuitangaza shule hiyo .
Diwani wa Kata ya Gongolamboto Lucas Lutainurwa aliwapongeza Walimu wa shule hiyo pamoja na wanafunzi ambapo walimu wa shule hiyo walipewa zawadi mbalimbali kwa ufaulu.
“Natoa pongezi na shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa shule pia nawapongeza walimu kwa jitihada zao kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyokusudiwa ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita “alisema Rutainurwa.
Diwani Lucas Rutainurwa alisema Walimu kazi yao ya wito pia ni ngumu lakini hawakati tamaa katika kusimamia taaluma shuleni mpaka kuzidisha ufaulu kwa shule hiyo wanafunzi wote wamepata alama A na alama B .
Aliwataka Wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao shuleni ili kuakikisha wote wanafaulu ili kuendelea na masomo ya ngazi ya juu .
Aidha aliwataka walimu wa shule ya sekondari Juhudi kuongeza juhudi katika kufundisha ili wanafunzi wapige hatua katika sekta ya elimu.
“Nawaomba walimu kuwa na ushirikiano pamoja na malengo ya kufanya vizuri kwa kufanya ufatiliaji wa karibu ikiwa ni kuweza kubaini wanafunzi wanakwama wapi katika taaluma kabla kufikia katika mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu kidato cha sita “alisema
Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Happiness Pallangyo amemshukuru Diwani Rutainurwa kwa kushiriki katika halfa hiyo, na kusema halfa hii iwe chachu kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.
“Hafla hii ni kwaajili ya kutambua juhudi na jitihada kubwa walizofanya walimu wetu kwenye mitihani ya kidato Cha sita mwaka 2024. Tunaamini tukio hili litaleta hamasa na chachu ya watu kujituma ili mwaka huu waweze kufanya vizuri zaidi” alisema Pallangyo.
Aliwataka walimu waliopata zawadi kutobweteka badala yake waendelee kujituma Zaidi kwa maendeleo ya shule hiyo ambapo mwaka huu imetia fora Juhudi Sekondari kwenye matokeo ya kidato cha 6 kwa Wilaya ya kwa kutia fora.
Mwalimu Pallangyo alisema matokeo ya mwaka huu kidato cha sita wanafunzi wamepata alama A na Alama B wanafunzi 96 wamepata Division 1 juhudi Sekondari Wilayani Ilala
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano