Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Malikale na kitabu cha historia ya asili ya Ukerewe kilichoandikwa mwaka 1895 na Mtanzania kutoka wilayani Ukerewe mkoani Mwanza,Anicet Kitereza vimekabidhiwa kwenye Chuo cha Mtakatifu Agustine Tanzania (SAUT) jijini Mwanza.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi malikale na kitabu hicho Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Colorado Denver kilichopo nchini Marekani Profesa, Charles Musiba ameeleza kuwa vitu hivyo vilikuwa vimehifadhiwa tangu mwaka 1968 kwenye chuo kikuu cha St.Olaf University Minnesota USA.
Musiba amesema malikale hizo zitahifadhiwa kwenye chuo cha SAUT ili kutoa elimu kwa wahitimu mbalimbali na watafiti ili waweze kuelewa historia ya Ukerewe na tamaduni zao.
Naye Makamu Mkuu wa chuo cha SAUT Profesa Costa Mahalu ameleeza kuwa licha ya kuhifadhi malikale hizo bado kuna umuhimu wa kutafuta kaburi lake ili kuweka historia itakayowasaidia watafiti kuandika historia yake.
“Mali kale hizi tutazitumia kuhamasisha wageni kutembelea kwenye chuo chetu cha SAUT kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa kabila la Wakerewe na zitarahisisha wanafunzi wanaofanya utafiti kuhusu kabila la Wakerewe kupata taarifa,” ameeleza Profesa Mahalu.
Malikale zilizorejeshwa katika chuo cha SAUT ni pamoja na picha za asili ya Mkerewe, shoka, nakala za kitabu kilichoandikwa na Kitereza kwa lugha ya Kikerewe chenye jina “Bwana Nyombekele na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulihwali, wamekabidhi barua za Kitereza alizokuwa anamwandikia rafiki yake mzaliwa wa Marekani, Gerald Hartwig ambaye ni mtafiti katika Sayansi ya Utamaduni (Anthropology).
Pia ala za muziki wa kabila la Wakerewe ikiwemo Nanga, vifaa vya kuandalia chakula, jembe lililotengenezwa kwa kuyeyusha chuma kwa njia ya asili iliyotumiwa na kabila hilo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi